COPA AMERIC: MESSI AFUNGA BAO 1 NA KUSAIDIA BAO 2 KUIPELEKA ARGENTINA KATIKA FAINALI

Mwanasoka bora wa dunia Lionel Messi ameibuka shujaa kwa timu yake ya taifa ya Argentina baada ya kuiongoza katika ushindi wa bao 4-0 dhidi ya Marekani katika mechi ya nusu fainali ya Copa America Centenario.


Ezequel Lavezzi alitangulia kuipatia Argentina bao la kwanza dakika chache tu baada ya kuanza mchezo huo akitumia vyema pasi ya Messi kisha Messi akafunga bao la pili kwa njia ya mpira wa adhabu ndogo.

Kipindi cha pili Mshambuliaji Gonzalo Higuain alifunga magoli mawili na kukamilisha ushindi wa bao 4-0 walioupata Argentina katika michuano ya mwaka huu nchini Marekani.

Messi amefikisha magoli 55 aliyeifungia Argentina na kumfanya kuwa mchezaji pekee aliyefunga mabao mengi kwa nchi hiyo akiwa na timu ya Taifa.

Argentina imetinga katika fainali ya michuano hiyo kwa mara ya pili mfululizo ikisubiri mshindi wa mechi ya nusu fainali ya pili kati ya  mabingwa watetezi Chile na Colombia mchezo utakaopigwa usiku wa kuamkia kesho huku fainali ikipigwa Jumatatu



No comments

Powered by Blogger.