YAMETIMIA: MAN UNITED YAMTIMUA VAN GAAL,MOURINHO ATAJWA KURITHI MIKOBA

Louis van Gaal kocha mkuu wa Mashetani wekundu  wa Old Trafford klabu ya Manchester United ametimuliwa katika nafasi hiyo uamuzi uliokua ukitegemewa na Wapenda Soka wengi wengi duniani.




Van Gaal mwenye miaka 64 amedumu na  United Kwa miaka miwili tu katika mkataba wake wa miaka mitatu ambao ulitarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu ujao.

Nafasi ya kocha huyo sasa iko wazi na wadadisi wa maswala ya soka wanamtaja aliyekua kocha wa Chelsea Jose Mourinho kuwa ndiye atakayerithi mikoba ya Van Gaal huku akitegemewa kutangazwa kesho Jumanne baada ya kuonekana akiwa na viongozi wa Manchester United.

Maurinho ameshinda ubingwa wa Ligi kuu England mara 3 akiwa na Chelsea mwaka 2005,2006 na 2015.

MAMBO UNAYOPASWA KUYAJUA 

Manchester United imefunga magoli 49 tu msimu huu ikiwa ni mara ya kwanza tangu msimu wa 1989/1990.

Ushindi wa kombe la FA Jumamosi iliyopita umewapa Man United kombe la kwanza tangu alipooondoka Sir Alex Ferguson mwaka 2013.

Man United imepiga pasi za nyuma (Backwards pass) 3,222 katika ligi.

Van Gaal ametumia wachezaji 33 msimu huu kiwango ambacho ni kikubwa zaidi akitanguliwa na Liverpool waliotumia wachezaji 34.

Man Utd imekua timu ya kwanza kupata clean sheets nyingi kuliko timu yoyote katika ligi kuu ya England sawa na Arsenal zote zikiwa na clean sheet 18.

No comments

Powered by Blogger.