WINGA WA ARSENAL NJE MIEZI MIWILI KUIKOSA PIA MICHUANO YA EURO 2016
Winga wa kimataifa wa England Anayeichezea Arsenal Alex Oxlade-Chamberlain atakua nje kwa muda wa wiki 6 mpaka 8 kutokana na maumivu ya goti.
Hii ni mara ya pili msimu huu kwa Mchezaji huyo kupata maumivu ya goti baada ya kukaa nje kwa muda mrefu mwanzoni mwa mwaka huu wakati Arsenal ilipocheza na Barcelona katika ligi ya mabingwa barani Ulaya.
Bosi wa Arsenal Arsene Wenger amesema mchezaji huyo mwenye miaka 22 ambaye ameichezea England mara 24 atakuwa nje kwa takribani miezi hiyo miwili na kukosa si tu mechi zilizobaki kwa Arsenal lakini pia atazikosa fainali za Mataifa ya Ulaya mwaka huu yanayotarajia kuanza Juni 10 mwaka huu huko Ufaransa.

No comments