TIMU ZOTE ZA TANGA ZASHUKA DARAJA, SIMBA YACHAPWA TENA,AZAM NA YANGA WAAMBULIA SARE
Heka Heka za ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara zimekamilishwa leo kwa timu zote kucheza Mechi za mwisho ambazo zimetoa timu mbili zilizoungana na Coastal Union kushuka daraja.
Jiji la Tanga limepoteza timu zake zote za ligi kuu na kufanya jiji hilo kukosa uwakilishi kwa msimu ujao wa ligi kuu baada ya African Sports na Mgambo JKT kuungana na Coastal Union leo kushuka daraja.
Ikicheza ugenini mjini Manungu African Sports ililambishwa bao 2-0 na wenyeji Mtibwa Sugar wakati Mgambo wakitoka sare ya bao 1-1 na Azam FC
Katika michezo mingine leo Simba ikiwa jijini Dar es Salaam ilikubali kichapo cha bao 2-1 toka kwa JKT RUVU ushindi ambao umewahakikishia maaskari hao kubaki katika ligi msimu ujao.
Mabingwa Yanga wakicheza katika Mchezo wao wa ugenini mjini Songea walienda sare ya bao 2-2 na wenyeji Maji Maji ya huko.
Kagera Sugar wakiwa nyumbani katika dimba la Kambarage waliwafunga Mwadui kwa bao 2-0 ushindi ambao umewahakikishia Kagera kubaki ligi kuu.

MATOKEO YA MECHI ZOTE ZA LEO.
- Azam FC 1-1 Mgambo JKT
- JKT Ruvu 2-1 Simba SC
- Maji Maji 2-2 Yanga SC
- Kagera Sugar 2-0 Mwadui FC
- Mtibwa Sugar 2-0 African Sports
- Toto Africans 0-1 Stand United
- Mbeya City 0-0 Ndanda FC
- Prisons 2-0 Coastal Union
No comments