SARE YA MAN CITY NA ARSENAL YAISAFISHIA MAN UNITED TOP 4

Zikiwa zimebakia mechi 2 kwa baadhi ya timu huku zingine zikibakiza mechi 1 kumaliza msimu huu wa mwaka 2015/2016 katika ligi kuu ya England huku pia Bingwa akishapewa kombe lake sasa vita imebaki katika Top 4 na kushuka Daraja.


Manuel Pellegrini akiwaaga mashabiki wa Man City jana
Sare ya bao 2-2 baina ya wenyeji Manchester City na Arsenal imewapa ahueni Manchester United kuingia katika Top 4 kwani sasa kama watashinda mechi zao mbili zilizobaki wanafikisha pointi 69 ambazo zitaishusha Man City na Arsenal (I wapo Arsenal wanafungwa mechi ya mwisho)

Manchester United imebakiza mechi 2 ya kwanza ikiwa dhidi ya West Ham kesho na ule wa mwisho dhidi ya Bournemouth huku Manchester City wao wakibakiza mechi ya mwisho dhidi ya Swansea ugenini wakati Arsenal wao wamebaki na mechi moja dhidi ya Aston Villa

Msimamo wa ligi umebaki hivi Leicester City wao ni Mabingwa wakiwa na pointi 80 hivi sasa wakati Tottenham Hotspurs wakiwa na pointi 70 katika nafasi ya pili. Arsenal wana pointi 68 katika nafasi ya 3 huku Man City wao wakishika nafasi ya nne wakiwa na pointi 65 timu zote hizi zimebakiza mechi 1 wakati Man United wao wako nafasi ya 5 wakiwa na pointi 63 na michezo miwili mkononi.

Kwa upande wa timu zinazoshuka Daraja baada ya Aston Villa kushuka Daraja zimebaki timu 2 za kuungana na Aston Villa na timu tatu zinataka kujikwamua na balaa hilo Sunderland,Newcastle na Norwich hizi ndizo ziko katika balaa hilo.

Norwich City ikiwa imebakiza michezo miwili inakamata nafasi ya 19 ikiwa na pointi 31 wamebakiza mchezo dhidi ya Watford kesho kutwa na mchezo wa mwisho dhidi ya Everton

Kwa upande wa Newcastle United wao wanakamata nafasi ya 18 baada ya Sare yao ya juzi ya bila kufungana na Aston Villa wana pointi 34 wakiwa na mchezo mmoja tu wa kuwaokoa dhidi ya Tottenham Hotspurs

Sunderland wao baada ya ushindi wa juzi dhidi ya Chelsea sasa wana nafasi kubwa ya kubaki katika ligi kwani wana pointi 35 katika nafasi ya 17 wakibakiza michezo miwili mmoja ukiwa kesho kutwa dhidi ya Everton na ule wa mwisho dhidi ya Watford.

MATOKEO YA MECHI ZA JANA EPL

  • Man City 2-2 Arsenal 
  • Liverpool 2-0 Watford 
  • Tottenham 1-2 Southampton 

No comments

Powered by Blogger.