RONALDO AFUNGA PENATI YA MWISHO NA KUIPA MADRID UBINGWA WA 11

Cristiano Ronaldo alipiga penati yamwisho iliyoipa Real Madrid ubingwa wa 11 wa michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya wakiwafunga ndugu zao Atletico Madrid Kwa penati 5-3.



Mechi hiyo ya Fainali ilipigwa katika dimba la  San Ciro jijini Milan Italia ambapo timu hizo zilimaliza dakika 90 kwa sare ya bao 1-1.

Nahodha Sergio Ramos alitangulia kuifungia Real Madrid dakika 15 ya mchezo akiunganisha mpira wa faulo uliopigwa na Toni Kroos lakini Yanick Carasso aliisawazishia Atletico Madrid bao dakika ya 78 na kufanya mchezo huo kumalizika Kwa sare ya bao 1-1.

Licha ya kuongezwa dakika 30 lakini bado hakuna aliyeona lango la mwenzake na ndipo changamoto ya mikwaju ya penati ikatumika kuamua bingwa wa msimu huu.

Beki wa Atletico Guafran ndiye mchezaji pekee aliyekosa penati yake jana usiku baada ya mpira aliopiga kugonga mwamba na  ndipo Cristiano Ronaldo alipoenda kumalizia penati ya mwisho iliyowapa ushindi Madrid na kuendelea kutawala kama timu pekee iliyochukua ubingwa mara nyingi zaidi

Ubingwa huo umekua ni mafanikio makubwa ya kocha mpya Zinedine Zidane ambaye ameifundisha Real Madrid kwa miezi 5 tu na kuingia katika historia ya makocha waliolitwaa kombe hilo kama wachezaji name makocha akifata nyayo za Pep Guadiola na Carlo Ancelott

Tumekuwekea hapa highlights za  mchezo huo pamoja na sherehe za kukabidhiwa Ubingwa.

HIGHLIGHTS ZA MCHEZO


KUKABIDHIWA UBINGWA

No comments

Powered by Blogger.