ROONEY AWEKA REKODI MAN UNITED IKIIKANDAMIZA BOURNEMOUTH

Nahodha wa Manchester United Wayne Rooney jana aliweka rekodi nyingine baada ya kufunga bao lake la 100 katika ligi kuu ya England katika dimba la Old Trafford pekee akiwa ni mchezaji wa pili kufanya hivyo baada ya Thierry Henry aliyefunga mabao 114 katika dimba la Highbury.



Rooney aliyocheza jana kama kiungo alifunga bao la kwanza katika ushindi wa bao 3-1 walioupata Manchester United dhidi ya AFC Bournemouth  katika dimba la Old Trafford

Kazi nzuri ya Antony Martial upande wa kushoto akipiga krosi na Rooney kuuweka mpira kambani bao ambalo lilidumu mpaka mapumziko.

Marcus Rashford alifunga bao la pili kabla ya Ashley Young hajafunga bao la Tatu dakika chache baada ya kuingia uwanjani akichukua nafasi ya Antony Martial lakini Chris Smalling alijifunga wakati akijaribu kuokoa mpira zikiwa sekunde chache mpira kumalizika.

Mechi hiyo ya jana ilikua ni ya kukamilisha ratiba baada ya kushindwa kufanyika Jumapili kutokana na sababu za kiusalama.

Kama hukupata muda wa kuangalia mechi hiyo Wapenda Soka blog tumekuwekea hapa highlights

No comments

Powered by Blogger.