RASMI : JOSE MOURINHO ATAMBULISHWA RASMI KAMA KOCHA MKUU WA MANCHESTER UNITED
Siku tatu za kufatilia mkataba wa Kocha Jose Mourinho zimehitimishwa kwa taarifa rasmi kutoka katika mtandao wa klabu ya Manchester United ikimtangaza rasmi Jose Mourinho kama Kocha mkuu wa klabu hiyo.
Jose Mourinho ambaye ameshashinda vikombe 22 tangu mwaka 2003 anachukua nafasi ya kocha Loius Van Gaal aliyetimuliwa baada ya kumalizika kwa fainali za kombe la FA ambapo United walitawazwa kama mabingwa mara ya 12.
Mourinho ataanza kazi rasmi baada ya michuano ya Euro 2016 na amesaini mkataba wa miaka mitatu wenye kipengele kinachomruhusu kukaa katika klabu hiyo hata baada ya mwaka 2020
José Mourinho mwenye miaka 53, amefundisha soka kwa zaidi ya miaka 10 katika ngazi ya juu barani Ulaya akishinda makombe katika nchi zote alizopitia zikiwemo Ureno,England, Italia na Spain
Amefanikiwa kushinda ubingwa wa ligi ya mabingwa barani Ulaya mara mbili akiwa na Porto mwaka 2004 na Inter Milan mwaka 2010.
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Manchester United Ed Woodward ndiye aliyetangaza uteuzi wa kocha huyo na kusema "Jose ni kocha bora katika nyakati tulizonazo ameshinda makombe na kuwezesha mafanikio ya wachezaji wengi barani Ulaya na zaidi ya yote anaielewa vyema ligi kuu ya England akishinda makombe mara 3 katika ligi hiyo, nachukua nafasi hii kumkaribisha katika klabu yetu rekodi yake ya kubeba makombe ni silaha tosha ya kuipeleka klabu mbele" alisema Ed.
Kwa upande wake Mourinho yeye alikua na haya ya kusema " Kuwa kocha wa Manchester United ni heshima kubwa kwangu kwani ni klabu inayojulikana na kupendwa duniani kote kuna kitu cha kipekee katika klabu hii ambacho hakuna klabu nyingine inayoweza kukifikia" alisema Jose Mourinho.
Aliendelea kusema "Nimekua na kumbukumbu nzuri ndani ya Old Trafford na siku zote nimekua nikipendezwa na mashabiki wa United hivyo basi nategemea kuwa meneja wao nikitegemea kuungwa mkono zaidi"
Mourinho alitimuliwa na Chelsea mwishoni mwa mwaka jana baada ya matokeo mabaya na tangu kipindi hicho amekua akihusishwa kuhamia.

No comments