MECHI YA KWANZA KWA RASHFORD AKIWA NA TIMU YA TAIFA YA ENGLAND LEO DHIDI YA AUSTRALIA
Mshambuliaji chipukizi wa England na klabu ya Manchester United Marcus Rashford leo atacheza mechi yake ya kwanza akiwa na kikosi cha timu yake ya taifa ya England.
Rashford anatazamiwa kuanza katika mechi ya leo ya kirafiki dhidi ya Australia katika dimba la Mwangaza nyumbani kwa Klabu ya Sunderland.
Kufuatia kuumia kwa Daniel Sturadge kunampa Rashford mwenye miaka 18 nafasi ya kucheza katika kikosi huku Kocha wake Roy Hodgson akiwaambia waandishi wa Habari kwamba dunia yote inasubiri kuona nini ambacho Rashford atafanya leo.
Hii ni mechi ya pili ya kirafiki kwa England baada ya kuibuka na ushindi katika mechi ya wiki iliyopita wa bao 2-1 dhidi ya Uturuki ikitazamiwa kucheza mechi nyingine wiki ijayo dhidi ya Ureno kabla ya kuanza kwa michuano ya kombe la mataifa ya Ulaya Euro 2016.

No comments