MABINGWA LEICESTER CITY WAFUNGA MITAA YA BANGKOK KUSHEREKEA UBINGWA

Mabingwa wa Ligi kuu nchini England Leicester City wameanzia Thailand katika kusherekea ubingwa wao walioutwaa msimu huu wakikusanya maelfu ya mashabiki katika paredi ya wazi katika mitaa ya Bangkok nchini Thailand.


Nchi hiyo ya bara la Asia ni nyumbani kwa wamiliki wa timu hiyo Vichai na Aiyawatt Srivaddhanaprabha.

Kikosi chote cha kocha Claudio Ranieri kimejumuika katika sherehe za ubingwa huko Bangkok Thailand na wakiwa katika jiji hilo walipata heshima ya mapokezi makubwa wakiwa katika bus la wazi wakiwa na kombe la ubingwa wa England.

Zaidi ya mashabiki 240,000 walijitokeza njiani kuwalaki na zaidi ya mashabiki 100,000 walikusanyika uwanja wa wazi wanawake,wanaume na Watoto katika tamasha kubwa la kuwapongeza.

Hii ni mara ya pili Leicester City kufanya hivyo mara ya kwanza ikiwa ni pale walipopanda Daraja lakini hii ya sasa imevunja rekodi baada ya maduka na biashara zote kufungwa kwaajili ya kusherekea ubingwa.


No comments

Powered by Blogger.