LEO KATIKA HISTORIA : REAL MADRID YABEBA UBINGWA WA 9 UCL MWAKA 2002

Leo katika Historia tunakumbuka fainali ya ligi ya Mabingwa barani Ulaya baina ya Real Madrid na Bayer Leverkusen  iliyofanywa tarehe kama ya leo yani tarehe 15 Mei 2002 katika dimba la Hampden Park jijini Glasgow Scotland.

Real Madrid walifanikiwa kushinda mchezo huo kwa ushindi wa bao 2-1 na kushinda ubingwa wao wa 9 katika historia ya michuano hiyo 

Raul alikua wa kwanza kuifungia Real Madrid bao dakika ya 8 ya mchezo likiwa bao lake la 34 katika michuano hiyo lakini bao hilo halikudumu sana kwani dakika 5 baadae beki wa kati wa Bayer Leverkusen Lúcio aliisawazishia Leverkusen kwa mpira wa Kichwa. 

Dakika ya 45 mpira wa krosi ya beki wa pembeni wa Real Madrid Roberto Carlos ulimkuta Zinedine Zidane aliyeunganisha bila kutuliza kwa kombora kali lililojaa kimiani na kuwapa ubingwa wao wa 9 katika mashindano hayo.

Bayer Leverkusen wao licha ya kupoteza katika fainali hiyo walipata faraja kwa kushinda ubingwa wa Ligi kuu nchini Ujerumani Bundesliga.

    VIKOSI

Bayer Leverkusen:
 Butt, Zivkovic, Lucio (Babic 90), Placente, Basturk, Ballack, Schneider, Sebescen (Kirsten 65), Ramelow, Neuville, Brdaric (Berbatov 38). 

Wachezaji wa Akiba ambao hawakutumika : Juric, Vranjes, Dzaka, Kleine.

Real Madrid: 
Cesar (Casillas 68), Salgado, Carlos, Hierro, Zidane, Helguera, Solari, Makelele (Flavio 73), Raul, Morientes, Figo (McManaman 61). 
Wachezaji wa Akiba ambao hawakutumika : Guti, Karanka, Munitis, Pavsn.

Watazamaji: 52,000

Refa: Urs Meier (Switzerland).

No comments

Powered by Blogger.