KUELEKEA KATIKA PAMBANO LA STARS NA MISRI ELNENY NA SALAH WAITWA KATIKA KIKOSINI.

Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars itapambana na Mafarao timu ya taifa ya Misri Juni 4 mwezi ujao jijini Dar es salaam katika kuwania nafasi ya kufuzu kwaajili ya fainali zijazo za kombe la mataifa ya Afrika zitakazofanyika Gabon mwakani.

Kuelekea katika pambano hilo kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Misri Hector Cuper ametangaza kikosi cha wachezaji 25 akiwajumuisha nyota kadhaa wanaokipiga ligi mbali mbali barani Ulaya akiwemo kiungo wa Arsenal Mohamed ElNemy na winga wa AS Roma Mohamed Salah 


Katika kundi G ambalo Taifa Stars na Misri wapo Mafarao hao wanaongoza kundi hilo wakiwa na pointi 7 wakati Nigeria wana pointi 2 na Stars tuna pointi 1 hivyo basi Misri watahitaji pointi moja tu kupata nafasi ya kushiriki michuano hiyo.

KIKOSI KAMILI CHA MISRIMakipa:

 Essam El-Hadary (Wadi Degla),Sherif Ekrami (Ahly) na Ahmed El-Shennawy (Zamalek)

Mabeki: 

Ahmed Fathi (Ahly), Mohamed Abdel-Shafy (Saudi Ahly), Hazem Emam (Zamalek), Ahmed Hegazy (Ahly), Rami Rabia (Ahly), Sabry Rahil (Ahly), Ali Gabr (Zamalek),Ayman Ashraf (Smouha), Hamada Tolba (Zamalek) na Karim Hafez (Omonia)


Viungo: 

Abdullah El-Said (Ahly), Hossam Ashour (Ahly), Mohamed Elneny (Arsenal),Mohamed Salah (Roma), Mohamed Ibrahim (Zamalek), Tarek Hamed (Zamalek), Mohamed Hassan 'Trezeguet' (Anderlecht), Moemen Zakareya (Ahly) na Amr Warda (Panetolikos)


Washambuliaji:

 Marwan Mohsen (Ismaily), Ahmed Hassan 'Kouka' (Braga) na Amr Gamal (Ahly)

No comments

Powered by Blogger.