RASMI: CONTE ATANGAZWA KUWA KOCHA MPYA WA CHELSEA NI MUITALIANO WA 5 KUIFUNDISHA "THE BLUES"
Baada ya uvumi wa muda mrefu hatimaye Chelsea imemtangaza kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Italia Antonio Conte kama kocha wake mpya baada ya kukamilisha taratibu za mkataba jijini London.
Conte mwenye miaka 46 amesaini mkataba wa miaka mitatu kuwafundisha Mabingwa hao watetezi wa taji la Ligi kuu nchini England na ataanza kazi rasmi baada ya kumalizika kwa mashindano ya Euro 2016 ambapo atakua na timu ya taifa ya Italia katika fainali zitakazofanyika Ufaransa.
Kwa sasa Chelsea itaendelea na Guus Hiddink, ambaye amechukua nafasi ya Jose Mourinho aliyetimuliwa ambaye atadumu na timu hiyo mpaka mwisho wa msimu.
Conte anakua kocha wa tano kuifundisha Chelsea baada ya Gianluca Vialli, Claudio Ranieri, Carlo Ancelotti na Roberto Di Matteo.
Conte ameiongoza Juventus kushinda ubingwa wa Italia mara tatu mfululizo kati ya mwaka 2011/2012 na 2013/2014 kabla hajatimkia timu ya taifa ya Italia.

No comments