WAKATI MAN UNITED NA LIVERPOOL ZIKISHINDA, MAN CITY,ARSENAL NA TOTTENHAM ZAAMBULIA VICHAPO
Mzunguko wa 28 wa ligi kuu nchini England umemalizika kwa majonzi na furaha kwa Mashabiki wa soka ikitegemeana na timu unayoshabikia.
Tottenham Hotspur wameshindwa kutumia nafasi adimu ya kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo kama ingeshinda baada ya kukubali kichapo cha bao 1-0 toka kwa West Ham goli pekee likifungwa na Michail Antonio.
Liverpool wakiwa nyumbani Anfield waliikandamiza Manchester city bao 3-0 ikilipa kisasi cha kufungwa na Man City katika kombe La Capital one Jumamosi.
Magoli ya Liverpool yalifungwa na Adam Lallana, James Milner na Roberto Firminho katika mechi ambayo Manchester city walipiga mashuti mawili tu yaliyolenga lango huku Liverpool wakipiga mashuti 7.
Manchester United wakiwa nyumbani OLD Trafford waliitandika Watford kwa bao 1-0 bao pekee La Mpira wa adhabu ndogo iliyopigwa na Juan Mata dakika ya 83 na kuendeleza wimbi La ushindi kwa Manchester United ambayo inatumia wachezaji wengi chipukizi hivi sasa kutokana na kukabiliwa na majeruhi wengi kikosini
Arsenal wakiwa nyumbani uwanja wa Emirates Jijini London walikubali kichapo cha bao 2-1 toka kwa Swansea ambayo inapigania kutoshuka Daraja msimu huu. Arsenal walitangulia kupata bao lililofungwa na Joel Campbell kisha Swansea kusawazisha kupitia kwa Wayne Routledge na badae nahodha Ashley Williams akifunga bao lake ushindi.
Katika mechi nyingine Stoke waliifunga Newcastle United bao 1-0 na Kuzidi kuiporomosha Newcastle katika hatari ya kushuka Daraja.

No comments