RONALDO APIGA BAO LA 90 REAL MADRID IKITINGA ROBO FAINALI
Cristiano Ronaldo jana alifunga bao lake la 90 katika historia ya ligi ya Mabingwa barani Ulaya wakati Real Madrid ikiifunga AS Roma bao 2-0 na kutinga robo fainali ya michuano hiyo mikubwa kwa ngazi ya klabu barani Ulaya.
Real Madrid imetinga Robo fainali kwa ushindi wa Jumla wa bao 4-0 baada ya kushinda Mechi ya awali kwa Idadi hiyo hiyo ya bao 2-0 huku Ronaldo akipiga bao 2 katika mechi hizo mbili.
James Rodriguez alifunga bao la pili baada ya Ronaldo kutangulia kufunga katika mechi hiyo iliyopigwa katika dimba La Santiago Bernabeu jijini Madrid.
Goli moja alilofunga Ronaldo jana linamfanya kuwa mchezaji pekee aliyefunga magoli mengi zaidi katika historia ya ligi ya Mabingwa barani Ulaya pia ni goli lake la 40 msimu huu katika mashindano yote na ni goli lake la 13 katika michuano ya ligi ya Mabingwa barani Ulaya msimu huu.
Licha ya kufunga bao hilo Ronaldo alizomewa na mashabiki wa Real Madrid baada ya kukosa nafasi nyingi zaidi wazi Kipindi cha kwanza.
Katika mechi nyingine hiyo jana wenyeji Wolfsburg waliitandika Gent ya Ubelgiji kwa bao 1-0 na kutinga hatua ya Robo fainali kwa ushindi wa Jumla wa bao 4-2.

No comments