MWANZILISHI WA SOKA LA "KAMPA, KAMPA TENA" AFARIKI DUNIA
Gwiji na mwanzilishi wa Total Football duniani ambayo waswahili wameipa jina la "Kampa kampa tena" ambayo inatumiwa sana na klabu ya Barcelona ya Hispania Mdachi Johan Cruyff amefariki dunia akiwa na miaka 68.
Cruyff, aliyeiwahi kuzichezea klabu za Barcelona, na Ajax pamoja na timu ya taifa ya Uholanzi amefariki leo asubuhi jijini Barcelona Spain alikolazwa akisumbuliwa na matatizo ya kansa.
Cruyff aliiongoza Uholanzi mara 48 na kufunga mabao 33 akiiongoza pia timu yake hiyo ya taifa kufika katika fainali za kombe la dunia mwaka 1974 na kupoteza kwa bao 2-1 dhidi ya Ujerumani Magharibi.
Mafanikio makubwa aliyopata Cruyff na hatasahaulika ndani ya Barcelona sio tu uwezo wake wa kuingiza staili ya "kampa kampa tena" lakini pia kushinda ubingwa wa Ulaya mara moja na ubingwa wa La Liga mara 4 kwa kipindi cha miaka 8 aliyoifundisha Barcelona.
Licha ya mafanikio hayo Barcelona walimtimua baada ya kushindwa kufanya vizuri zaidi na mpaka anatimuliwa mwaka 1996 Cruyff akishinda Jumla ya vikombe 11.
Cruyff ameshinda pia Tuzo ya mchezaji bora wa dunia Balon D'or mara 3 akishinda mwaka 1971,1973 na 1974.
![]() |
Cruyff akimkabidhi jezi Rais Kikwete alipokuja nchini. |

KWA KIFUPI HIKI NDICHO ALICHOFANYA CRUYFF WAKATI WA UHAI WAKE.
KAMA MCHEZAJI
- Ajax (1964-73) – Michezo 240 akifunga magoli 190.
- Barcelona (1973-78) – Michezo 143 magoli 48.
- LA Aztecs (1979-80) – Michezo 23 magoli 13.
- Washington Diplomats (1980-81) – Michezo 30 magoli 12
- Levante (1981) – Michezo 10 magoli 2.
- Ajax (1981-83) – Michezo 36 magoli 14.
- Feyenoord (1983-84) – Michezo 33 Magoli 11.
- Holland (1966-77) – Michezo 48 Magoli 33.
KAMA KOCHA
- Ajax (1985-88)
- Barcelona (1988-96)
- Catalonia (2009-13)
MAFANIKIO
KAMA MCHEZAJI
- Dutch titles: 9
- Dutch Cups: 6
- Spanish titles: 1
- Copa del Reys: 1
- European Cups: 3
KAMA KOCHA
- Spanish titles: 4
- Copa del Reys: 1
- European Cups: 1
- Dutch Cups: 1
- Cup Winners Cups: 1
Nice
ReplyDelete