MESSI APIGA HAT- TRICK BARCELONA IKIIPIGA RAYO BAO 5
Mbio za ubingwa kwa Barcelona zimezidi kuongezeka baada ya jana kutoa kipigo cha bao 5-1 kwa Rayo Vallecano Katika mwendelezo wa ligi KUU nchini Spain La Liga.
Mara nyingi haihitaji timu inayocheza na Barcelona iwe pungufu ili Barcelona ishinde yani Hata timu pinzani ikiwa timilifu bado kuwafunga Barcelona huwa ni tatizo sasa kwa jana Rayo Vallecano iliwabidi kuwakabili Barcelona wakiwa 9 baada ya kutolewa wachezaji wawili na Hali ikawa mbaya kwa timu hiyo ambayo ilikua ikicheza katika uwanja wa nyumbani.
Ivan Rakitic alitanguLia kufunga bao la kwanza kisha Lionel Messi akafunga bao la pili na kufanya mchezo huo kwenda mapumziko Barcelona wakiwa mbele kwa bao 2-0.
Kipindi cha pili Barcelona waliongeza bao la tatu kupitia kwa Lionel Messi tena kabla ya Manucho hajaifungia Rayo bao la kufutia machozi na Messi akaongeza bao la nne huku Arda Turan akifunga bao la tano na la kwanza kwake akiwa na Barcelona.
Messi sasa amefikisha mabao 20 katika mechi 16 za La Liga msimu huu na pengine Messi angefunga bao la 21 kama angeamua kupiga mwenyewe penati ambayo Barcelona waliipata na Luis Suarez kushindwa kufunga.
Matokeo mengine katika la Liga jana Granada waliifunga Sporting Gijon bao 2-0 wakati Real Betis wakisafiri ugenini waliinyuka Espanyol bao 3-0.

No comments