LUKAKU AJIPIGIA CHAPUO KUSAJILIWA MAN UNITED ASEMA HANA TATIZO KUFANYA KAZI TENA NA MOURINHO

Mshambuliaji wa Ubelgiji na klabu ya Everton ya England Romelu Lukaku anayewaniwa na Manchester United amefunguka na kusema haoni shida kufanya kazi tena na Jose Mourinho.



Wapenda Soka blog iliripoti wiki hii kwamba Baba yake Romelu Lukaku amemshauri mwanae ajiunge na moja kati ya klabu mbili Bayern Munich ya Ujerumani au Manchester United ya England kwaajili ya msimu ujao wa ligi.

 Mourinho na Lukaku walikua pamoja katika kikosi cha Chelsea na kocha huyo aliamua kumuuza Mshambuliaji huyo msimu uliopita kwa kile kilichoelezwa kwamba hakua amefikia kiwango cha juu alichokihitaji.

'Watu wanaweza kusema natakiwa kumshawishi ili aniamini lakini sio kweli kwani miaka mitatu iliyopita nilikua na miaka 20 na Sikua tayari kuwa bora katika kiwango cha juu cha kucheza katika timu kubwa'

'Misimu miwili bora kwangu imeshapita tangu kipindi hicho ikiwemo msimu huu na Mambo yamebadilika. Nitakua na miaka 23 ikifika  Mei na kila kitu kitakua sawa' alisema Lukaku alipozungumza na mtandao wa Derniere Heure.

Alipoulizwa kuhusu alichosema baba yake kuhusu kujiunga na Bayern Munich au Manchester United Lukaku alisema ' Najua kwanini alisema vile kwakua wakati nikiwa mdogo Bayern Munich na Manchester United ndizo zilikua timu zinazonivutia jinsi walivyokua wana safu bora za ushambuliaji na inakua vizuri kwangu kuona nafatiliwa na vilabu hivi kilichobaki ni kwa wakala wangu kukamilisha mipango'

Lukaku amefunga magoli 45 katika mechi 85 tangu aliposajiliwa rasmi na Everton miezi 20 iliyopita.



No comments

Powered by Blogger.