KOMBE LA FA : PALACE YATINGA NUSU FAINALI LEO NI EVERTON NA CHELSEA
Mechi za hatua ya Robo fainali ya kombe la Chama cha soka nchini England FA zilianza jana katika uwanja wa Madejski jijini Reading England.
Crystal Palace inayonolewa na Allan Pawdew ikiwa ugenini iliweza kuibuka na ushindi wa bao 2-0 magoli ya kipindi cha pili ya Yohan Cabaye kwa njia ya penati na lile moja la Fraiser Campbell dakika za mwisho za mchezo huo ambao kipa wa Reading Al Habsi aliibuka shujaa baada ya kucheza mipira mingi sana iliyolenga lango.
Leo katika jiji la Liverpool wenyeji Everton watakua nyumbani katika dimba La Goodson Park kuwaalika Chelsea katika mechi ambayo inavuta hisia za Wapenda Soka duniani kutokana na ubora wa vikosi vyote
Chelsea inajivunia kutinga hatua hii kwa ushindi mnono wa bao 5-1 dhidi ya Manchester city wakati Everton wao wametinga hatua hiyo kwa kuifunga Bournemouth bao 2-0.
Mechi Baina ya timu hizo itaanza saa 2 na nusu usiku kwa saa za Afrika Mashariki.

No comments