FALSAFA ZA KROENKE NA MWENENDO MBAYA WA ARSENAL

Kuna mengi yananiumiza kichwa kuhusu Arsenal, Bodi inawazaga ubingwa kweli??? Na huwa inamalengo hayo?? Hata kwenye vikao vyao huwa wanaiweka hiyo agenda??? Haya ni maswali ambayo rafiki yangu mmoja shabiki wa kutupwa wa Arsenal alikuwa anauliza.


Stan Kroenke
Tufahamu kuwa tatizo  lililopo katika bodi ya Arsenal ni kwamba hakuna ata mtu mmoja ambae ana ujuzi wowote kuhusu mpira labda ujuzi kidogo sana kuhusu mpira. Naweza sema labda yule Mkurugenzi mtendaji Bwana Ivan Gazidis (ambaye naye taaluma yake ni mwanasheria) ila kwa sababu amekaa kwenye mambo ya mpira wa miguu kwa muda mrefu anaweza kuwa na elimu kidogo juu ya mpira wa miguu. Afu yeye ndo mdogo kuliko wote ana miaka 51 hapo

Ivan Gazidis
Na wakati Ivan Gazidis anachaguliwa kua Mkurugenzi Mtendaji wa Arsenal, mzee wetu Arsene Wenger alikuwa ni mmoja wa wajumbe walihidhuria kikao cha kumchagua , Kwa iyo Ivan Gazidis ambae ni Mkurugenzi ni ngumu kumadhibu au kumsema Wenger kuwa anakosea (wakati ni kitu ambacho anatakiwa kukifanya kama bosi)

Waliobaki wengine ni wazeee wazeee yani wana miaka 80 na 70 yani hawajawahi ata kucheza mpira ule wa makaratasi. Na wazee hawa wamekuwa Arsenal kwasababu ya urithi wa kifamilia ambayo ilikua ni utamaduni wa Arsenal. Hivo ndivyo walivokua mashabiki wa arsenal.


Alisher Usmanov 
Ni mtu mmoja tu tena ni Mrussuia mzee Usmanov ndiyo amekua analilia apewe share kubwa. Ndiyo huwa anasikika kuhusu kusajili na anaonekana kama ana upenzi na timu. Lakini ana 30% ya hisa za Arsenal kwa hiyo hana uamuzi wowote zaidi ya kuchangia mada tu.


Wengine ndo wale wamarekani  Stan kroenke na mwanae Josh Kroenke huyu ana miaka 35 tu. Stan kroenke  mwenye umiliki wa hisa nyingi pale Arsenal. Kwa hiyo ndiyo mwenye maamuzi yote makubwa. Kuhusu mambo ya hela, kufukuza watu na mengineo

Mwaka 2015, Stan Kroenke alimuita mwanae Josh Kroenke awe mmoja wa waunda bodi ya Arsenal. Josh ana miliki timu ya mpira wa kikapu, na ana miliki timu za farasi na timu ya mpira wa miguu wa Marekeani (American Football)

Josh Kroenke
Naongea kwa kujiamini kabisa kuwa huyu jamaa hana mapenzi yoyote na Mpira wa miguu, yuko Arsena kwa sabab za kibiashara. Anajulikana kwa jina la utani "silent kroenke" kwa sababu haongeagi chochote kwenye vyombo vya habari yeye ni vitendo tu.

Kafika Arsenal na cha maana alichokifanya ni kupandika bei ya tiketi kwa 3% zaidi japokua hata kabla hajapandisha Arsenal ndIyo ilikua timu inayoongoza kwa kutoza bei kubwa ya tiketi kwenye ligi zote duniani za kandanda.

Cha ajabu zaidi ni kuwa hiyo 3% iliyoongezeka kila mwisho wa mwaka huwa inaenda kwenye kampuni yake kama malipo kutoka Arsenal. Malipo ambayo wao wenyewe wanayaita "strategic and advisory services" Kinachokera mashabiki kwa nn iwe ile ile 3% ya ongezeko la bei ya tiketi ndiyo iingie kwenye akaunti ya Josh Kroenke.

Ukitaka kujua mahusiano yaliyopo kati ya bodi ya Arsenal chini ya Stan kroenke na Arsene Wenger

Hawa jamaa wanamuheshim sana Wenger. Mwaka 2002 bodi ya Arsenal ndo waliweka wazi mipango ya kujenga uwanja mpya wa Emirates (Jina kamili la uwanja wa Arsenal ni Ashburton)

Katika kujenga uwanja lazima muwe wabahili na kuminya bajeti. Walimwambia Wenger wazi mikakati yao kuwa kama atakubali kuendelea kuifundisha timu basi ataendesha timu kwa ndogo sana, kwa sababu nguvu zote zitaamishwa kwenye kujenga uwanja.

Na lengo lake kubwa walimpa ni kushika nafasi ya 4 ili waende UEFA mana kule kuna hela nyingi tu na za bure. Wenger alikubali mambo yakaanza, kilicho muadhibu Wenger ni kwamba muda huo anakubali kufanya haya na ndo watu kama wakina Roman Ambramovich (Chelsea ) wanaingia katika ligi kuu Uingereza na pia Alex Ferguson anaipaisha Manchester United kuwa moja ya timu kubwa ulaya na kuifanya timu kuwa na pesa nyingi sana. Kwa hiyo Wenger ndiyo akafifia kuanzia miaka iyo 2005 apo mpaka hapo juzi deni lilivoisha

Arsene Wenger
Kiukweli Wenger alifanya kazi kubwa sana. Ndiyo maana mpaka leo hii, bodi ya Arsenal haiwezi kunyanyua mdomo kutamka kumfukuza Wenger. Wenger ataondoka mwenyewe akitaka.

Kuanzia mwaka 2004 apo mpaka 2012 mwishoni, kauli mbiu ya Arsenal ilikua kuhaakikisha wanamaliza ndani ya nafasi nne za mwanzo na kuweka nguvu kwenye "Academy" na "Academy" hiyo hiyo ikiwa nzuri uza wachezaji Arsenal ipate hela. Pia kulikuwa hakuna kununua wachezaji wenye majina


Hapa ndiyo wapo watu kama Adebayor, Toure, Fabregas, Song, Van Persie na wachezaji kama Samir Nasri. Wenger alifanikiwa haya yote tena kwa Grade A. Ndiyo maana hawa jamaa hawawezi kumgusa Wenger

Wanamuamini, mambo yote yanayohusu mpira wamemwachia Wenger. Wenyewe wanahakikisha akaunti zinasoma faida ni kubwa huku Arsenal ikiendeshwa  kwa bajeti ndogo.

Mwaka 2013, deni la uwanja liliisha. Ndo kidogo Wenger akaanza kupata fungu la usajili Ozil, sanches, Petr Cech na wengineo wamesajiliwa kwenye mkumbo huo. Lakini tatizo sasa Wenger akili imeganda. Bado anaamini falsafa zake zile za miaka ile bado zitamsaidia.

Mambo yamebadilika, masuala ya usajiri yAmebadilika, mbinu za uchezaji mpira zimebadilika, mambo ya mitandao ya kijamii. Pamoja na mabadiliko haya yote ila Wenger amebaki yule yule.

Huu ndo ugonjwa sugu na ushakua sugu kweli kweli. Maana wale wakurugenzi kule juu wamekaa tu Na Wenger yeye anategemea miujiza tu. Mi mzee nafikiri apumzike tu. Apande cheo kwenye bodi aje kocha mpya mwenye mbinu mpya.

Na Frankinho - Member wa Wapenda Soka Tanzania

No comments

Powered by Blogger.