DABI YA LONDON KASKAZINI LEO NI TOTTENHAM VS ARSENAL
Mbio za ubingwa wa ligi kuu nchini England zinaingia katika hatua nyingine muhimu leo kwa timu mahasimu wa jiji la London Tottenham Hotspurs watakaokua nyumbani White Hart Lane kuwaalika Mabingwa wa kombe la FA Arsenal.
Tottenham walio katika kiwango kizuri kabisa hivi sasa wanakamata nafasi ya pili katika msimamo wanakutana na Arsenal ambao wako katika nafasi ya tatu katika msimamo.
Timu zote hizi zimetoka kufungwa katika michezo yao na zinatofautiana kwa pointi 3 tu Tottenham wakiwa na pointi 54 huku Arsenal wao wakiwa na pointi 51.
Golikipa wa Arsenal Petr Cech ataikosa mechi hii baada ya kuumia misuli ya mguu kwenye Mechi na Swansea na nafasi yake itachukuliwa na David Ospina. Pia Laurent Koscienly ataikosa mechi hii akisumbuliwa na maumivu.
Kwa upande wa Tottenham wao hawana majeruhi katika kikosi cha kwanza huku kiungo Mousa Dembele ambaye alitoka mechi iliyopita kutokana na majeruhi anatazamiwa kurejea leo.
UNACHOPASWA KUKIJUA
● Tottenham wamepoteza Mechi 1 tu kati ya mechi 7 zilizopita wakiwa kwao White Hart Lane dhidi ya Arsenal Wakishinda 4 na kutoka Sare 2
● Arsenal wameshinda Mechi ya mwisho katika uwanja wa White Hart Lane Mwezi Septemba 2015 kwenye Kombe la Ligi, Capital One Cup.
● Tottenham Hotspurs wanapigania kumaliza ligi wakiwa juu ya Arsenal hii ikiwa ni Mara ya kwanza tangu walipofanya hivyo mwaka 1995.
● Harry Kane amefunga magoli matatu katika mechi mbili za ligi dhidi ya Arsenal na amefunga magoli 13 katika mechi 17 za Dabi za London.
● Alexis Sanchez hajafunga goli lolote katika ligi kuu nchini England tangu Mwezi Oktoba mwaka jana goli pekee alilofunga hivi karibuni lilikua dhidi ya Hull city katika kombe La FA.

No comments