BECKHAM APANGA KUMPA UKOCHA ROBERTO CARLOS

Taarifa toka Nchini Spain zimeeleza kwamba David Beckham amemtaja Roberto Carlos kama mtu sahihi wa kuweza kuifundisha timu anayoimiliki ya Miami United  nchini Marekani.



Miami United inayoshiriki ligi kuu nchini Marekani maarufu kama MLS inamilikiwa na staa huyo wa zamani wa klabu ya Manchester United na amepanga kuiinua klabu hiyo kuanzia msimu wa mwaka 2017 akitaka pia kumsajili Lionel Messi siku za usoni.

 Beckham na Roberto Carlos walicheza pamoja wakiwa Real Madrid na Beki huyo wa zamani wa Real Madrid na timu ya taifa ya Brazil pengine angefurahia nafasi hii ya kuungana tena na Becks.

 Roberto Carlos hivi sasa anaifundisha timu ya Delhi Dynamos inayoshiriki ligi kuu nchini India akiwa ameshaifundisha pia klabu ya Anzhi Makhachkala ya Russia.




No comments

Powered by Blogger.