BABA YAKE ROMELU LUKAKU AMSHAURI MWANAE AJIUNGE NA BAYERN MUNICH AU MAN UNITED

Baba mzazi wa mshambuliaji wa Everton na timu ya Taifa ya Ubelgiji Romelu Lukaku aitwaye Roger  ametanabaisha kwamba ni wakati sasa wa mwanae kuihama Everton huku akiamini kwamba Bayern Munich na Manchester United ndizo zinazomfaa kwa maisha yake baada ya kutimka Everton.



Lukaku amekua na msimu mzuri ndani ya Goodson Park msimu huu akiwa ameshafunga mabao 25 katika mashindano yote Licha ya timu hiyo ya jiji la Liverpool kushindwa kufanya vyema Ikikamata nafasi ya 12 hivi sasa katika msimamo wa ligi kuu ya England.
Atletico Madrid, Bayern Munich, Juventus, Chelsea na Manchester United ndizo timu ambayo zimeonyesha nia ya kumwania kwa ajili ya msimu ujao huo huku mzee wake akiamini timu mojawapo kati ya Bayern Munich na Manchester United ni chaguo sahihi kwa mwanae.
'Nadhani anatakiwa kuchagua kati ya Manchester United au Bayern Munich. Manchester United ni timu inayojengwa upya na kwa umri wake angefaa zaidi pale na Bayern Munich ingefaa kwake kama Roberto Lewandowski ataihama klabu hiyo.

No comments

Powered by Blogger.