AZAM YAIPUNGUZA KASI YANGA MABINGWA MATOKEO YA MECHI ZOTE ZA VPL JANA

Mabingwa watetezi  wa ligi kuu nchini Tanzania Yanga SC jana wamepunguzwa kasi na Azam FC kwa kalazimishwa Sare ya bao 2-2.
Yanga kabla ya kukutana na Azam FC ilishinda michezo mitatu mfululizo ikiwa ni pamoja na ushindi wa bao 2-0 dhidi ya Simba.

Mlinzi wa Yanga Juma Abdul alijifunga na kuwapa Uongozi Azam kabla ya Mlinzi huyo hajarekebisha makosa yake kwa kufunga bao la kusawazisha kisha Donald Ngoma akafunga bao la pili kabla ya John Bocco hajaisawazishia Azam na kufanya mchezo huo kumalizika kwa Sare hiyo ya bao 2-2.

Simba leo itacheza mchezo wake dhidi ya Mbeya City na kama ilishinda itazipiku Azam FC na Yanga kwani itafikisha pointi 48 huku Azam na Yanga zikiwa na pointi 47.

MATOKEO YA MECHI ZOTE ZA JANA VPL

  • Azam FC 2-2 Yanga SC 
  • Toto African 0-0 Ndanda FC 
  • Mtibwa sugar 3-0 Coastal Union 
  • Kagera Sugar 1-1 Mgambo JKT 
  • Prisons FC 1-0 Stand United 
  • JKT Ruvu 1-0 Mwadui FC 

No comments

Powered by Blogger.