SIMBA YATUMBULIWA JIPU NA YANGA TAIFA
Furaha ya ushindi katika mechi 7 mfululizo kwa Wekundu wa Msimbazi Simba zimefikia hatamu leo baada ya kukubali kichapo cha bao 2-0 toka kwa mahasimu wao na watani wa jadi Yanga
Kadi ya pili ya njano aliyopata mlinzi wa Simba Abdi Banda kisha kutolewa kwa kadi nyekundu dakika za Mwanzo kabisa za mchezo ilidhoofisha kikosi cha kocha Jackson Mayanja na kupelekea kuzidiwa mno katika mechi hiyo.
Donald Ngoma wa Yanga alitangulia kufunga bao la kwanza dakika ya 39 baada ya makosa ya mlinzi wa Simba Hassan Kessy kushidwa kumpa mpira kipa wake Angban na mpira kuna wa na Ngoma ambaye alifunga kuulaini na kufanya mchezo huo kwenda mapumziko matokeo yakiwa ni bao 1-0.
Kipindi cha pili kilikuwa kichungu zaidi kwa Simba kwani walionekana kukosa umakini na kupoteza hovyo mipira hali iliyowapa nafasi Yanga na kupata bao la pili dakika ya 72 likifungwa na Amiss Tambwe baada ya kumzidi ujanja Juuko Murshid aliyeshindwa kuokoa mpira wa krosi uliopigwa na Mwashiuya.
Kwa matokeo hayo Simba inashuka mpaka nafasi ya 3 baada ya Azam kushinda huku Mbeya bao 3-0 wakiifunga Mbeya City hivyo kulingana kwa pointi wote wakiwa na pointi 45

No comments