MESSI APIGA 2 BARCELONA WAKIIFUNGA ARSENAL KWAO, JUVENTUS NA BAYERN SARE

Mechi za kwanza za hatua ya 16 bora ya ligi ya mabingwa barani Ulaya ziliendelea tena jana usiku katika viwanja viwili jijini London England na Juventus kule Italia.



Mchezaji bora wa dunia hivi sasa Lionel Messi akiwa na kikosi cha Barcelona waliibamiza Arsenal bao 2-0 katika Mchezo uliopigwa katika dimba la Emirates jijini London.

Messi Alifunga mabao yote mawili kipindi cha pili moja akifunga Kwa kumalizia pasi murua ya Neymar huku la pili akifunga Kwa penati baada ya Methieu Flamin aliyeingia kuchukua nafasi ya Francis Conquelin kumwangusha Messi katika eneo la hatari  na mwamuzi kuamuru ipigwe penati ambayo ilifungwa na Messi

Katika mechi nyingine hiyo jana Juventus wakiwa nyumbani iliwalazimu kusawazisha magoli mawili ambayo Bayern Munich walitangulia kufunga.

Mpaka mapumziko tayari Bayern Munich walishafunga bao moja kupitia Kwa Thomas Mueller kabla ya Arjen Robben hajaongeza la pili kipindi cha pili na ndipo Juventus wakastuka na kuanza kusawazisha kupitia Kwa Paul Dyabala na Sturaro

Mechi za marudiano zitapigwa baada ya wiki ijayo ambapo washindi watatinga hatua ya Robo fainali.

No comments

Powered by Blogger.