MAN UNITED NA STOKE, ARSENAL WANYEJI WA WATAKATIFU, LIVERPOOL MDOMONI MWA LEICESTER

Ligi kuu nchini England inaendelea usiku wa leo kwa mechi 8 kupigwa katika viwanja tofauti nchini humo.



Vinara wa ligi hiyo Leicester City wao watakuwa  Nyumbani kuwakabili Liverpool chini ya kocha Juggen Klopp katika dimba la King Power

Ni msimu ambao hakuna aliyetabiri  Leicester kuwa juu wakati huu tunaingia mwezi February ikiwa na pointi 47 wakati Liverpool wao wana pointi 34 katika nafasi ya saba.

Jijini Manchester  wenyeji Manchester United chini ya kocha Louis van Gaal watakua wakiwakaribisha Stoke City inayotolewa na mshambuliaji wa zamani wa Manchester United Mark Hughes.

United itaingia katika mchezo wa leo ikiwa na pointi 37 katika nafasi ya Tano ikiwa imepoteza mchezo uliopita dhidi ya Southampton katika ligi wakati Stoke wao wanakamata nafasi ya 9 wakiwa na pointi 33 huku mchezo uliopita wakipoteza dhidi ya Leicester katika ligi kuu.

Arsenal wanaoshika nafasi ya 3 wakiwa na pointi 44 watakua nyumbani kuwakaribisha Southampton ambao hujulikana pia kama Watakatifu wanaokamata nafasi ya 8.

RATIBA KAMILI YA MECHI ZA LEO EPL



No comments

Powered by Blogger.