CHELSEA YAIKANDAMIZA MAN CITY 5 KOMBE LA FA, SPURS YATUPWA NJE NA PALACE


Chelsea jana wakiwa katika kiwango bora kabisa waliikandamiza Manchester City bao 5-1 katika pambano la hatua ya 5 ya michuano ya kombe la FA nchini England katika dimba la Stamford Bridge




Manchester City iliyotumia wachezaji wengi wa timu ya vijana ilifanikiwa vilivyo kuikamata Chelsea ambayo iliteremesha kikosi chake chote na mpaka mapumziko ubao ulisomeka sare ya bao 1-1 magoli ya Diego Costa na David Faupala.

Kipindi cha pili kilikua kigumu kwa Manchester City ambao wanakabiliwa na mchezo wa ligi ya mabingwa Ulaya wiki hii dhidi ya CSKA Moscow kwani waliweza kuruhusu mabao manne zaidi yakifungwa na Willian,Gary Cahill,Eden Hazard na Bertrand Traore na kufanya mchezo huo kumalizika kwa ushindi mkubwa wa bao 5-1 kwa Chelsea.

Katika michezo mingine hiyo Jana West Ham waliitandika Blackburn Rovers bao 5-1 katika mechi iliyopigwa katika dimba la Ewood Park. Victor Moses akifunga bao moja huku Dimitri Payet na Emmanuel Emenike wakifunga mabao mawili kila mmoja.

Tottenham wakiwa nyumbani walilala bao 1-0 toka kwa Crystal Palace goli pekee likifungwa na Martin Kelly baada ya kazi nzuri ya Wilfried Zaha.

Mechi ya mwisho ya mzunguko huo wa Tano itachezwa leo usiku ambapo Manchester United watakua ugenini kucheza na Shrewbury Town mchezo utakaoanza majira ya 5 kasorobo.

No comments

Powered by Blogger.