SIMBA YAZINDUKA MWISHONI NA KUTOA KIPIGO KWA BUKINABE MORO

Magoli matatu ya dakika za mwisho yameipa Simba SC ushindi muhimu dhidi ya Burkina Faso ya Morogoro katika mechi ya kombe La Shirikisho hatua ya tatu.



Pambano hilo lililomalizika kwa Simba kushinda bao 3-0 lilipigwa katika dimba la Jamhuri mjini Morogoro.

Hamis Kiiza alitangulia kuipa Simba bao dakika ya 77 baada ya kosakosa nyingi tangu kipindi cha kwanza huku tukishuhudia safu ya ushambuliaji ya Simba ikishindwa kabisa kupenya safu ya Ulinzi ya Burkina Faso. Kiiza alifanikiwa kufunga bao safi kwa kisigino akitumia vizuri pasi ya Abdi Baada.

Said Hamis Ndemla aliipatia Simba bao la Pili kwa shuti kali nje ya boksi na kumwacha kipa wa Burkina Faso asije la kufanya wakati mpira ukitinga wavuni.

Kiiza alifunga bao la tatu zikiwa zimebaki sekunde kadhaa tu mpira kumalizika kwa njia ya penati baada ya Said Ndemla kuangushwa kwenye penati boksi wakati akitaka kuuwahi mpira ili afunge na Hamis Kiiza bila ajizi akafunga bao lake la pili katika mashindano hayo likiwa ni goli la 12 msimu huu akiwa na Simba.

Kwa matokeo hayo Simba imetinga hatua ya nne ya michuano hiyo ambayo imerudi mwaka huu tangu mwaka 2002 ikidhaminiwa na Azam Media.

No comments

Powered by Blogger.