LIVERPOOL YATINGA FAINALI CAPITAL ONE KWA MATUTA

Kikosi cha Liverpool jana ilibidi kusubiri mpaka hatma yao kuamuriwa na upigaji wa penati ili kupata nafasi ya kucheza Fainali ya kombe la ligi nchini England maarufu kama Capital One.




Mpaka dakika 90 zinakamilika Stoke City walikua wakiongoza kwa bao 1-0 lililofungwa na mshambuliaji Marko Arnautovic na kufanya matokeo ya jumla kuwa sare ya bao 1-1 baada ya mechi ya awali pale Britania Liverpool kuibuka na ushindi pia wa bao 1-0.

Baada ya dakika 90 zikaongezwa nyingine 120 na matokeo yakabaki vile vile na ndipo changamoto ya mikwaju ya penati ikabidi kuamua mechi hiyo na ndipo Liverpool iliposhinda kwa penati 6-5 .

Waliofunga penati za Liverpool

Adam Lallana,Christian Benteke,Roberto Firmino,James Milner,Lucas Leiva na Joe Allen

Waliokosa kwa Liverpool

Emre Can


Waliofunga penati za Stoke City

Jonathan Walters,Glenn Whelan, Ibrahim Afellay,Xherdan Shaqiri na Marco Van Ginkel.

waliokosa kwa Stoke City

Peter Crouch na Marc Muniesa

Kwa matokeo hayo Liverpool itacheza Fainali tarehe 28 Februari na mshindi kati ya Everton na Manchester City ambao wanakutana leo

No comments

Powered by Blogger.