YANGA YAFANYA MAUAJI DAR, SIMBA YAKAMATWA MWANZA
Magoli matatu ya mshambuliaji Amiss Tambwe na bao moja la kiungo Shabani Kamusoko yalitosha kuimaliza timu ya Stand United ya Shinyanga katika pambano la Ligi kuuya Vodacom Tanzania bara.
Yanga ambayo inaongoza ligi hiyo imeibuka na ushindi huo mzito wa bao 4-0 katika mechi iliyopigwa katika dimba la Taifa Jijini Dar es Salaam ushindi ambao unazidi kuwaweka Yanga kileleni mwa ligi hiyo ikifikisha pointi 30.
Huko Jijini Mwanza Simba wameangukwa na machozi baada ya kukubali bao la kusawazisha la Toto Africa dakika za lala salama baada ya kutangulia kufunga bao moja kipindi cha kwanza hivyo mchezo huo kumalizika kwa sare ya bao 1-1
Daniel Lyanga alifunga bao safi la mapema kipindi cha kwanza ambalo lilidumu dakika zote za mchezo huku wengi wakiamini mpira ungeisha hivyo lakini dakika 4 za nyongeza ziliipatia Toto bao la kusawazisha likifungwa kwa kichwa na mshambuliaji Evarist Bernard.
No comments