WAPENDA SOKA DAY IMEWADIA, NI JANUARI 1, 2016

Hii ni siku maalumu ambayo wanachama na wapenzi wote wa Taasisi ya Wapenda Soka Tanzania waliridhia na kuipitisha iwe ni mahususi kwaajili ya kutoa misaada kwa jamii. Kwa Pamoja tulikubaliana siku hiyo kuwa JANUARI MOSI (TAREHE 1, JANUARY) Kila mwaka ambapo WAPENDA SOKA hujitolea chochote kile kwaajili ya kusaidia watu wenye uhitaji hasa WATOTO YATIMA na tumeweza kufanikiwa kufanya hilo kwa miaka mitatu sasa.

Mchakato wa kufanikisha Wapenda Soka Day ya mwaka 2016 umeshazinduliwa na Board ya muda ya Wapenda Soka Tanzania ambayo ilikutana jijini Dar Es Salaam na ahadi zimeshaanza kutolewa.

Ni wajibu wa kila mmoja wetu kutambua na kuthamini kile kidogo alichojaliwa na kusaidia jamii ya wenye Mahitaji.



Hivyo basi Ukiwa kama Mdau Mkubwa wa Kundi hili Tafadhali tunaomba mchango wako au ahadi ya kile ulichoguswa kutoa.

No comments

Powered by Blogger.