WAKINA SAMATA WAPOTEZA MECHI NYINGINE KLABU BINGWA YA DUNIA

Pambano la kutafuta mshindi wa 5 wa klabu bingwa ya dunia limemalizika mchana huu huko Osaka Japan kwa mabingaa wa Afrika klabubya TP Mazembe kuchapwa bao 2-1 na mabingwa wa CONCACAF Club America ya Mexico 



Dario Benedetto na Martin Zuniga walifunga magoli kwa upande Club America huku Rainford Kalaba akifunga bao la pekee la Mazembe na kufanya mchezo huo kumalizika kwa kichapo kwa mabingwa hao wa Afrika kutoka Congo. Huku Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu wakianza katika kikosi cha Tp Mazembe.
Badae leo mabingwa wa Amerika Kusini River Plate watapambana na mabingwa wa Japan Sanfrecce Hiroshima ambapo mshindi atacheza fainali na kati ya Mabingwa wa Ulaya Barcelona au mabingwa China Guangzhou Evergrande katika fainali itakayopigwa Jumapili hii.
Michunano hii hushirikisha mabingwa wa soka katika mabara 6 yaliyo chini ya FIFA pamoja na bingwa wa nchi mwenyeji 

No comments

Powered by Blogger.