SEPP BLATTER NA PLATINI " JELA" YA SOKA KWA MIAKA 8
Rais wa Fifa Sepp Blatter na Bosi wa Uefa Michel
Platini wamefungiwa kujihusisha na soka kwa miaka 8 kufuatia uchunguzi uliofanyika dhido yao.
Wakuu hao wa soka duniani wamekutwa na hatia ya matumizi mabaya ya ofisi na nafasi zao huku kukiwa na ufisadi wa paundi milioni 1.3 ambazo zilikua malipo kwa Platini mwaka 2011.
Adhabu dhidi yao inaanza mara moja na wote wawili wamekana kuhusika na wamepanga kukata rufaa.
Blatter mwenye miaka 79 amekua Rais wa FIFA tangu mwaka 1998, alishatangaza kuwa hatagombea tena Urais wa FIFA kwa awamu nyingine katika uchaguzi unaotaraji kufanyika mwezi February mwakani.
Plattini alikua anaonekana kama mtu sahihi kuiongoza FIFA baada ya Blatter. Platini amekua kiongozi wa Uefa Tangu mwaka 2007.
Licha ya adhabu hiyo Balatter na Platini wamepigwa pia faini ya paundi 33,700 Blatter na paundi 54,000 kwa Platini.
No comments