ROONEY NA ROJO KUZIKOSA WEST HAM NA WOLFSBURG

Wayne Rooney na Marcos Rojo watakosa michezo miwili ya Manchester United wa kwanza dhidi ya West Ham Jumamosi katika ligi na ule wa Ugenini dhidi ya Wolfsburg katika ligi ya Mabingwa Ulaya.



Akiongea na Waandishi wa habari leo kocha wa Manchester United Luois Van Gaal amesema Rojo ameumia bega wakati wa mazoezi juzi Jumatano na nahodha Wayne Rooney yeye anasumbuliwa na enka.

Katika mchezo uliopita Rooney alitolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Memphis Depay na kuna kila uwezekana sasa LVG akatafuta beki wa pembeni kushoto katika dirisha dogo kama Rojo hatapona mapema huku Luke Shaw akiendelea kuuguza mguu wake.

Phil Jones na Ander Herrera nao watakosa mechi ya Jumamosi dhidi ya West Ham lakini Jesse Lingard atarejea baada ya kupona maumivu ya misuli.

No comments

Powered by Blogger.