MERRY CHRISTMASS TOKA KWA DAVID OSPINA KIPA WA ARSENAL
Golikipa namba mbili wa Arsenal David Ospina ameshea picha yake akiwa na familia yake kupitia akaunti yake ya Instagram akiwatakia mashabiki wake sikukuu njema.
Katika picha hiyo Ospina yuko na Mkewe Jessica Sterling na aatoto wake wawili Dulce Maria ambaye ni mkubwa na Maximilliano ambaye ni mdogo.
Arsenal inakamata nafasi ya pili katika msimamo wa ligi kuu nchini England na mechi inayofata itakua Jumatatu ijayo dhidi ya Manchester City katika uwanja wa Emirates jijini London na ushindi utazidi kufufua matumaini ya kuchukua ubingwa wa ligi kuu msimu huu baada ya kuukosa kwa mwaka wa 10.
Usajili wa kipa Petr Cech kutoka Chelsea msimu huu kumemfanya Ospina kuwa chaguo namba mbili katika kikosi cha Arsene Wenger ambacho kimepangwa kucheza dhidi ya Barcelona katika mechi za hatua ya 16 bora katika ligi ya mabingwa barani Ulaya.
No comments