CHELSEA YALEYALE YACHAPWA TENA SAFARI HII NA LEICESTER CITY,MOURINHO ASHUSHA LAWAMA KWA WACHEZAJI


Huwezi kuamini lakini ni bora tu uamini Chelsea iliyokua tishio chini ya Jose Mourinho hivi sasa si lolote si chochote na inapigania kutoshuka daraja licha ya kuwa bingwa mtetezi wa ligi kuu nchini England.


Chelsea ikisafiri mpaka katika uwanja wa King Power nyumbani kwa Leicester City imeambulia kichapo cha bao 2-1 toka kwa vinara hao wa ligi kuu nchini England.

Jamie Vardy anayeongoza orodha ya wafungaji bora msimu huu alitangulia kuipatia Leicester City bao dakika ya 34 ya mchezo akitumia pasi murua ya Winga muAlgeria Riyad Mahrez na kufanya mchezo huo kwenda mapumziko Chelsea wakiwa nyuma kwa bao 1-0.

Dakika mbili baada ya kuanza kwa kipindi cha pili Riyard Mahrez aliichambua ngome ya Chelsea na kupiga shuti lililojaa wavuni na kuiandikia Leicester bao la pili kabla ya Loic Remy hajapata bao la kufutia machozi dakika ya 77.

Kwa matokeo hayo Leicester City imerudi kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 35 baada ya mechi 16 huku Chelsea ikipigania isishuke daraja kwa kubaki na pointi zao 15 katika nafasi ya 16 pointi moja juu ya mstari wa kushuka daraja.

Baada ya mchezo huo Kocha Jose Mourinho aliwatupia lawama wachezaji wake kwakusema wanachokubaliana mazoezini sio wanachokifanya uwanjani na ameenda mbali zaidi na kusema Chelsea imepoteza kabisa nafasi ya Top 4.

No comments

Powered by Blogger.