CAPITAL ONE CUP: MAN CITY NA EVERTON, LIVERPOOL KUWAKABILI STOKE CITY

Ratiba ya nusu fainali ya kombe la ligi nchini England Capital one imepangwa jana baada ya kumalizika mechi baina ya Liverpool na Wenyeji southampton ambapo Liverpool waliibuka na ushindi wa bao 6-1.


Manchester City ambao juzi waliifunga Hull City 4-1 wamepangwa kukutana na Everton ambao nao wamefika hatua hii baada ya kuiadabisha Midlesbrough bao 2-0 katika mechi za robo fainali.

Liverpool wao watakutana na Stoke City katika hatua hii ya nusu fainali mechi ambazo hazionekani kuwa rahisi kwa timu zote hizo nne kwani timu zote hizo ziko katika Ligi kuu ya England na zote zimeonekana kuwa na vikosi bora msimu huu.

Hatua ya nusu fainali huchezwa mechi mbili yani nyumbani na ugenini Mechi ya kwanza baina ya Everton na Manchester City itapigwa katika dimba la Goodson Park jijini Liverpool wakati Stoke watawakaribisha Liverpool katika mechi ya kwanza pale katika dimba la Britania.

Mechi za kwanza zitachezwa kati ya Januari 5 na 6 mwaka 2016 huku marudiano ikiwa ni Januari 26 na 27 mwaka 2016.






No comments

Powered by Blogger.