ANDIKO LA WAZI KWA EVANS ELIEZA AVEVA, RAIS WA SIMBA SPORTS CLUB.
Mheshimiwa Rais kwanza nikupe pole kwa majukumu mbalimbali ambayo unakabiliana nayo, na nikupongeze kwa jitihada nyingi unazozifanya kuhakikisha unapata mkate wa kila siku na timu yetu inaendelea kubaki Ligi kuu Tanzania.
Mheshimiwa nimelazimika kuchapisha andiko hili kama mdau wa michezo, na pengine wazo langu linaweza kugusa hisia za mashabiki na wanachama wa Simba ambao walikuunga mkono na kukupigia kura Tarehe 29 June mwaka jana pale Bwalo la Polisi ili uwe Rais mpya na wa kwanza wa timu yao, ninaguswa sana na haya yanayoendelea kwa sasa mitaani, vijiweni, mitandao na kwenye baadhi ya matawi ya wanachama wa Simba Sports Club.
Mheshimiwa Rais kwanza naomba tu nikukumbushe ulipotoka kabla sijaeleza madai haya ya wanachama yanayopigiwa kelele. Kabla ya kufanyika uchaguzi uliokuweka madarakani, timu ya Simba ilikuwa katika hali mbaya kiuchumi na kadhalika kimpira, ilikuwa ina miaka takribani miwili inavurunda katika ligi kiasi cha wewe mwenyewe (Aveva) na kundi zima la Friends of Simba kusema timu ilikuwa “Eda” na kwamba utakapoingia madarakani utaitoa Simba katika “Eda”
Tarehe 28 June, 2014 ukiwa unafunga kampeni zako katika ukumbi wa hoteli ya Hyatt Kilimanjaro huku ukiungwa mkono na watu wenye ushawishi mkubwa ndani ya club kama mwenyekiti wa zamani wa Simba Bw. Hassan Dalali, wanachama wenzio wa tawi la Friends of Simba Khasim Dewji, Zakaria Hans Poppe na wengine wengi, ulitoa ahadi na vipaumbele vyako mara tu utakaposhika hatamu ya uongozi, naomba nipitie ahadi zako kwa haraka haraka ambazo ulitumia kama karata na ukazichanga vililivyo.
SOKA LA VIJANA
Mheshimiwa Rais, uliahidi kuendeleza na kuwa na timu imara ya vijana chini ya miaka 20, hili lilikuwa ni hitaji kubwa kwa wanasimba wote hasa ukizingatia kwa wakati huo tayari walianza kunufaika na vijana wao kama Ramadhani Singano “Messi”, Harouna Chanongo, Jonas Mkude, Hamis Said Ndemla na wengineo. Na mimi ninakumbuka wakati wa utawala wa Hassan alikuteuwa Evans Aveva kuwa mwenyekiti wa kamati ya soka la vijana, hivyo ulikuwa unaelewa ulichokuwa unakiahidi kwasababu ulikuwa umekiishi. Hakuna mgombea ambae hakuguisa suala hilina mlitumia muda mwingi kulielezea katika kampeni zenu.

KUONGEZA WANACHAMA
Mheshimiwa ahadi yako hii wakati ukiielezea nakumbuka ulisisitiza kwamba Simba itakapokuwa inafanya vizuri wanachama wenyewe watarudi (waliondooka kutokana na timu kufanya vibaya) lakini itavutia wanacham wapya na hivyo kuwa na idadi kubwa ya wanachama ambao ni rasilimali nzuri kwa timu. Wakati unagombea Urais club ya Simba ilikuwa ina wanachama Takribani 7000 na ukaahidi kufikisha wanachama 50,000

UWANJA WA BUNJU
Mheshimiwa Rais hili lilikuwa fimbo yako kubwa ya kuwachapia wanyonge hawa waliojitokeza kusikiliza sera zako wakati wa kampeni, Huu ni mwaka wa Tisa wimbo wa Bunju haujachuja katika “playlist” yenu, ukiwa unaingia madarakani tulikuwa tumeusikia kwa miaka 7, ukianza na muasisi wake Hasan Dalali ambaye yeye angalau aliwezesha japo kupatikana kwa eneo, Ismail Aden Rage nae akauimba sana mpaka kufikia hatua akatoa siku 90 za kukamilisha uwanja ule ahadi ambayo hata mtoto mdogo hawezi kuipokea lakini kwa uvumilivu na utashi wa wanachama wa Simba walisubiri uwanja na haukutokea, bado na wewe ukaja na wimbo huohuo.

TIMU IMARA
Mheshimiwa Rais katika hili uliahidi kuwa na timu ya Simba imara na yenye ushindani ambayo ingechukua ubingwa na kutuwakilisha vema kimataifa. Mimi binafsi ninafahamu ile Simba “kiboko yao” ya miaka ya 2000 wewe ndio ulikuwa mwenyeketi wa kamati ya usajili, Aveva ni wewe uliwavumbua wakina Juma Kaseja, Boniface Pawasa, Ulimboka Mwakingwe, Emmanuel Gabriel na wengine wengi, hii ilikuwa ni kazi yako na timu ilikuwa tishio. Ahadi nyingine inayofanana nah ii ni usajili mzuri na timu kuwika katika Anga za Kimataifa.

Mheshimiwa tunafahamu uchaguzi wa Tarehe 29 june 2014 uligubikwa na mizengwe mingi kiasi cha Kamati ya Rufaa ya TFF kupokea rufaa mbalimbali na iliwalazimu Simba kusubiri mpaka TFF watoe uamuzi. Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya Simba, wakili Damas Ndumaro alitangaza kuenguliwa kwa jina la mgombea wa nafasi ya urais aliyekuwa na nguvu kubwa bwana Michael Richard Wambura hapo hali ya hewa ikaanza kuchafuka.
Wambura aliahidi kusitisha utegemezi katika club hii, hasa kutokana na timu kuyumba pale wafadhili wanapokuwa na tofauti za kimaslahi. Pengine hapa Wambura aliwalenga Friends of Simba ambao wamekuwa wakiiendesha timu kama mali yao, kuingia kwa Wambura ingekuwa ni mwisho wa ubabe huu wa FOS juu ya timu hii, likaundwa zengwe na Wambura akaenguliwa na kubaki wagombea wawili tu katika nafasi ya urais, ambao ni wewe (Aveva) na Andrew Tupa.
Zakaria Hans Poppe ambae ni “memba” wa friends of Simba na alijulikana sana kwa msaada wake kwa timu hii na fedha zake alizotumia kuhudumia timu pamoja na kulipa mishahara, alisikika akisema amechoka kuhudumia timu isiyofanya vizuri na kama wanachama hawatawachagua Evans Aveva na Geofrey Nyange basi atajitoa kufadhili timu hii, hii ina maana kwamba katika kura ulizopata zipo pia za watu walioogopa Simba “kufa njaa” na haikuwa demokrasia, mliyatafuta madaraka kwa nguvu kubwa.
Mheshimiwa Rais inawezekena unawafahamu wanasimba kwa unyenyekevu wao na uvumilivu wao ndio maana uliamua kuingia madarakani na ahadi za uongo ambazo hujatekeleza hata moja kwa utimilifu wake. Tangu umeingia soka la vijana limekufa, umeua soka hili ili Friends of Simba muendelee kuitawala Simba na kufanya usajili ambao kimsingi hauna manufaa kwa club. Zakaria Hans Poppe ambae “amekuweka” madarakani kwa jeuri ya pesa zake ndio anaonekana kama Rais wa club hii.
Wanachama umeshindwa kuwaongeza kwa njia uliyoiahidi (ya timu kufanya vizuri) matokeo yake yaananzishwa matawi mapya yanayoiba wanachama wa matawi mengine, unaongeza nini hapo mheshimiwa? Umeingia mkataba na EAG na kuwahadaa wanasimba kwamba sasa timu itajiendesha kibiashara lakini ni uongo wa wazi kabisa. Wewe na kamati yako wote mliongea mambo matamu ili kuwateka wapiga kura na kutishia kutoendelea na ufadhili ikiwa hautaingia madarakani.
IMETOSHA AVEVA
Wanachama wanaitaka timu yao, wanataka mafanikio yao na heshima yao. Wanahitaji uhuru wa nafsi na usafi wa fikra, wanataka furaha ya moyo na amani ya mpira. Wapo wanachama mliowapiga marufuku kukanyaga mako makuu ya Club kutokana na kujitambua kwao na kudai haki yao. Uongozi wako Aveva umeitafuna Simba na kuinyong’onyeza zaidi, umeifanya Simba kuwa dhaifu sana na masikini zaidi kutokana na muda unavyokimbia. Wanachama sasa wanamkumbuka Michael Richard Wambura na maneno yake, mmeifanya Simba iwategemee nyinyi kwa kila kitu, mmezifunga fikra na sauti za maamuzi kwa kushikilia uchumi wa club, hapana INATOSHA AVEVA.
Mohammed Enterprises Limited chini yake Mohammed G. Dewji wameifadhili na kuidhamini Simba kwa muda mrefu sana wakati ambao haikuwa rahisi kwa timu ya Tanzania kujiendesha kibiashara, lakini kwa dunia ya leo na fursa za kibiashara zinaongezeka kuna ulazima wa timu kutoka katika utegemezi kandamizi kama wa Friends of Simba na iwe huru kwa utegemezi wenye faida. Simba haihitaji wafadhili tena bali inahitaji wadhamini kwanza na uongozi wenye muundo mzuri wenye kuleta manufaa. Mohammed Dewji “MO” amekuja wakati muafaka kabisa na wanasimba wanahitaji kwa wakati huu, Simba hawana muda wa kukusubiri mpaka utoke madarakani, hawasubiri uonevu na ukandamizi uendelee, wanaitaka timu yao, INATOSHA AVEVA.
Bado wanasimba wanadai haki yao kwa unyenyekevu mkubwa huku wakiishangilia timu yao, Aveva usisubiri nyongo iwatumbukie ndani ili uone sura halisi za watu hawa unaowaongoza, mashabiki wa Simba sio wadhaifu na wala usithubutu kufikiri unaweza kuzima sauti zao, hapa walipofika hawatarudi nyuma tena!! Na kamwe usiwalazimishe wabadili utaratibu wa kudai haki yao hasira zao unazifahamu na ndio hasa unachokitazamia. Aveva mmegeuka kuwa wakoloni weusi, manawageuza wanasimba “mapoyoyo” wasiojua lolote.. Aveva, Aveva, Aveva usipime kina cha bahari kwa kidole, wasikilize wanachama wanataka nini, wape hitaji la moyo wao ambao wewe umeshindwa na umefeli kulitimiza, wape haki yao utawaonea mpaka lini? INATOSHA AVEVA
Simba haikuhitaji jezi mpya, haikuhitaji kadi mpya, ilichohitaji ni timu bora, imara, na yenye ushindani. Ilihitaji pia kuwa na timu nzuri ya vijana, ilihitaji kuona fedha zinazotoka kwa wadhamini zinachanganuliwa matumizi na kuleta maendeleo. Aveva hata rangi kopo moja imekushinda kupaka lile jingo kweli utauweza uwanja wa Bunju? Kwanini mnawafanya Simba wendawazimu na nyinyi ndio mna akili? Mabadiliko ya soka la kisasa wanayaona yatatokana na biashara, na tayari mfanyabiashara mkubwa ameamua kuwekeza kwanini msiachie?? Kama malengo yenu na malengo ya “MO” ni kuinua Simba kwanini mnakataa? Nini kinakufanya ung’ang’anie timu kama si kulipua hasira za wanachama? INATOSHA AVEVA
Nimalizie andiko langu kwa kukutakia Heri ya Christmas na mwaka Mpya, lakini kabla hujasherehekea sikukuu hizi kwanza uwape zawadi wanachama wa Simba kwa kukubaliana na mapendekezo ya Mohamed Dewji ili mwaka mpya kweli uwe na mambo mapya.
Jeff Gemo Mnyama Mashine
No comments