UCHAMBUZI: CHELSEAVS ASTON VILLA


Chelsea fc na Aston villa  wamekutana mara 143 lakini katika mechi hizo ,Chelsea fc kafanikiwa kuibuka na ushindi mara 58.
Wakati Aston villa yeye kafanikiwa kuibuka na ushindi mara 52 .
Pia wametoka sare mara 33 ,uku pia Aston villa akifanikiwa kufunga mabao 208 wakati Chelsea fc wao wakifanikiwa kufunga mabao 225 katika mechi hizo zote walizokutana .

Kwa mara ya kwanza Chelsea fc na Aston villa walikutana msimu wa 1938/1939

Je wajua Aston villa alishawai kuifunga Chelsea fc mabao 7-1 ilikuwa,ni msimu wa 1951/1952 napia Chelsea fc ikaja kulipa kisasi kwa kumfunga Aston villa bao 8-0 ilikuwa,ni msimu wa 2012/2013 .


Na ayo ndo matokeo makubwa,yaliyo wai kutokea,baina ya hizo timu mbili kati ya Chelsea fc na Aston villa


NGUVU ZA TIMU ZOTE MBILI NA UDHAIFU WAO

Chelsea fc ambao ni mabingwa watetezi wa ligu kuu ya uingereza ukiwatazama wanavyocheza utadahani bado wapo pre -season timu nzima imechoka lakini pamoja na timu kuchoka,lakin udhaifu mkubwa unaonekana upo zaidi kwenye safu ya ulinzi .


Mfano beki wa kulia mserbia ivanovic anaonekana kabisa amechoka na kasi imepungua pia kwa kiasi kikubwa .

Hivyo hivyo kwa mserbia mwenzake Nemanja matic moja kati ya viungo bora wa ukabaji kwa soka la sasa na yeye pia anaonekana kachoka kutokana na msimu uliopita kufanya kazi kubwa sana ndo mana msimu huu wale wachezaji waliokuwa bora,na muhimu kwa upande wa chelsea fc kwa,msimu uliopita ila  msimu huu wameonekana wamechoka  ukimtazama Eden hazard,Cesc,Diego costa,Ivanovic,Matic nk .

Kocha Jose Mourinho anachotakiwa sahivi kuwapa nafasi zaidi vijana wadogo kama kina loftus cheek,kenedy,baba rahman nk ili waweze kupata uzoefu uku tukiendelea kuamini kuwa wakongwe kuna muda watarudi kwenye ubora wao ili timu isipate matokeo mabovu sana damu changa kusaidiana na wakongwe ndo moja kati ya vitu ambavyo mourinho anatakiwa kufanya ili kunusuru kibarua chake.

Nyota wa mchezo huo kwa upande wa Chelsea fc nadhani na bado naamini ataendelea kuwa mbrazil Willian ambaye toka msimu huu uanze amezidi kuonyesha uwezo mkubwa hata pale timu inapokuwa imezidiwa kaifungia timu yake ya taifa juzi goli mbili katika ushindi wa goli 3-1 walioupata. Na pia kaendelea kuwa ndo mfungaji wa magoli mengi msimu pale darajani akiwa kafunga mabao manne katika mashindano yote uku mabao matatu kati ya ayo akiyafunga kwa kutumia mipira ya adhabu ndogo .



Japo chelsea fc watakuwa na furaha ya kumkaribisha nyota wao Diego costa  ni baada ya kumaliza ile adhabu yake ya kufungiwa mechi tatu kwasababu ya kumpiga kiwiko beki wa kati wa arsenal Laurent Koncienly .

Aston villa ni timu ambayo ukiitazama wanavyocheza wanaonekena bado hawana jipya msimu huu sijui ni kwasababu  hawakufanya usajili wa maana sana msimu huu na pia wamekuwa,na majeruhi kadhaa uku pia wamemuuza nyota wao Christian benteke  kwenda liverpool lakini pamoja na ayo sio timu ya kubeza hata kidogo mana siku zote Aston villa anapocheza na Chelsea fc lazima moto uwake ni kutokana na villa kuwa,na wachezaji wenye kasi sana kama kina Gabriel Agbonlahor ,Scott Sinclair,nk .

Wakati huo huo Aston villa,nao wanatatizo kama la chelsea fc japo wao sio sana .

Tusije shangaa mechi hii goli zikafungwa,nyingi kulingana na ubovu wa  beki za timu zote mbili uku pia Aston villa wao wakiongozwa na beki wawili wa zamani wa klabu ya Man city Micah Richards,na Jeloen Lescott nk.

Vikosi vinavyotarajiwa kuanza kwa pande zote mbili kama vilivyoripotiwa,na vyanzo mbali mbali ni kama ifuatavyo

Chelsea fc begovic  azpilicueta,cahill,zouma,baba rahman,Loftus Cheek,cesc fabregas,pedro,willian,diego costa,hazard

Kocha jose mourinho

Mfumo ni 4-2-3-1

Aston villa, Guzan,Richards,Lescott,Alan Hutton,Jordan Amavi,Jose Angel Crespo,Idrissa Gueye,Ashley Westwood,Rudy Gestede,Scott Sinclair,Jordan Ayew

Kocha Tim sherwood

Mfumo 3-5-2
Utabiri wa mechi

Chelsea fc 2 Aston villa 1

asanteni wenu mchambuzi

George james ballack

No comments

Powered by Blogger.