SIMBA NA AZAM SASA KUPIGWA DECEMBER
Mechi za raundi ya 11 za Ligi
Kuu ya Vodacom zilizokuwa zichezwe Novemba 7 na 8 mwaka huu sasa zitafanyika
Desemba 12 na 13 kupisha maandalizi ya Taifa Stars ya mechi za mchujo za Kombe
la Dunia.
Taifa Stars inatarajia kuingia kambini mapema mwezi ujao
kujiandaa na mechi ya kwanza dhidi ya Algeria ambayo itafanyika Novemba 14
mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Timu hizo zitarudiana nchini
Algeria, Novemba 17 mwaka huu.
Mechi hizo za Vodacom zitakazochezwa Desemba 12 ni kati
ya Mgambo Shooting na Yanga (Tanga), Kagera Sugar na Ndanda (Tabora), Stand
United na Mwadui (Shinyanga), Mbeya City na Mtibwa Sugar (Mbeya), Azam na Simba
(Dar es Salaam) na Majimaji na Toto Africans (Songea). Mechi za Desemba 13 ni
kati ya JKT Ruvu na Tanzania Prisons (Dar es Salaam), na Coastal Union na
African Sports (Tanga).
Pia mechi tatu za raundi ya sita ambazo hazikuchezwa
Oktoba 4 mwaka huu kupisha mechi ya Taifa Stars na Malawi sasa zitafanyika
Desemba 16 mwaka huu. Mechi hizo ni kati ya Azam na Mtibwa Sugar (Dar es
Salaam), na African Sports na Yanga (Tanga), mchezo kati ya Ndanda na Simba
(Mtwara utapangiwa tarehe ya kuchezwa.
Nayo mechi namba 59 kati ya JKT Ruvu na Mtibwa Sugar
iliyokuwa ichezwe Oktoba 21 mwaka huu Uwanja wa Karume, Dar es Salaam
imesogezwa mbele kwa siku moja hadi Oktoba 22 mwaka huu ili kuipa nafasi ya
mapumziko JKT Ruvu ambayo jana (Oktoba 18 mwaka huu) ilicheza mechi yake ya
raundi saba mkoani Shinyanga
No comments