KIJIWE CHA WAPENDA SOKA : TATHMINI ARSENAL VS MAN UNITED


Kijiweni leo Wapenda Soka wamefunguka kuhusu mechi ya Arsenal watakaokua nyumbani kuwakabili Manchester United katika uwanja wa Emirates jijini London 
Na haya ni baadhi tu ya maoni yao

King Mwesi: 

Blind asicheze mbali na Walcott, najua Darmian atammiliki Sanchez, Morgan amgasi Carzola akate mawasiliano kati yake na Coq
Man Utd3 Arsenal 1

Messi Msangi: 

Hapa bhana pana maneno mengi sana lakini pia kuna majigambo ya kila namna kwa mashabiki wa vilabu hivi ingawa upande mmoja huonekana kulemewa na kejeli za hapa na pale nawazungumzia mashabiki wa Manchester United majigambo yao kwa mashabiki wa Arsenal.

  Kumbuka kwa wewe mshabiki wa kati ya vilabu hivi  kwa mara ya kwanza kabisa timu hizi zilikutana 13/10/1894 kipindi hicho Manchester walijulikana kama Newton Heath na Arsenal wakitambulika kama Woolwich Arsenal na kwenye mchezo huo walitoka sare ya kufungana 3-3.

Sasa timu hizi zimekutana mara 221 safari hii itakuwa mara 222 na mara hizo 221 Manchester United wameibuka na ushindi mara 93 Arsenal wakishinda mara  79 na tukashuhudia sare 49  kwa maana hiyo Arsenal anatafuta ushindi wa 80, Manchester United wanatafuta ushindi wa wa 94 au pengine tukashuhudia sare ya 50.

Mchezo wa mwisho walipo kutana tulishuhudia sare ya 1-1 lakini kumbuka kipigo kikubwa zaidi pindi timu hizi zilipo kutana Arsenal alipokea kichapo cha goli 8-2 ilikuwa ni tarehe 28/8/2011 mchezo ambao umekuwa ukiwatesa sana mashabiki wa Arsenal mpaka leo.

Ni mchezaji mmoja tu aliebaki ambae anauwezo wa kuboresha zaidi rekodi yake ya kufumania nyavu pindi timu hizi zikikutana si mwingine bali ni Rooney ambae mpaka sasa anagoli 9 akiwa kinara.

  Arsenal wapo nafasi ya 4 wakiwa na pointi 13 wakati Manchester United wapo kileleni kwa mara ya kwanza baada miaka 2 wakiwa na pointi 16.
Sasa kuelekea katika mchezo huu ambao umekuwa na matokeo ya upande mmoja kwa maana hata kama Manchester United hawafanyi
vyema basi pindi wakikutana na Arsenal kumekuwa na mteremko.

Safari hii hali ya mambo ipo kinyume kwa maana katika misimu miwili Manchester United haikuwa vyema ukilinganisha na Arsenal
lakini bado walikuwa na uhakika wa kupata matokeo mbele ya arsenal tunaona msimu huu kikosi cha Van Gaal licha ya kwamba bado kinatafuta ubora kama ule wa enzi ya Ferguson lakini wamekuwa na matokeo mazuri kuliko wapinzani wao kikosi cha Wenger ambacho bado hatuoni mabadiliko yoyote.

Tunaiona Arsenal ambayo nafasi ya kiungo mkabaji ni tatizo na kumekuwa hakuna mawasiliano mazuri kati ya safu ya beki za kati
na kiungo kwa maana hiyo pasipo marekebisho kwa kuangalia kiwango kizuri cha Martial na Mata tutazungumza mengine.

Van Gaal kuelekea mchezo huu huku akiwa na kumbukumbu nzuri
ya kutokufungwa na Arsenal katika mara mbili walizo kutana katika
ligi nadhani marekebisho kwa upande wake ni katika beki kujisahau
hapa na pale lakini kwa asilimia kadhaa anauwezo wa kupata
matokeo mbele ya Arsenal.
Miaka 19 ya Mzee Wenger licha ya mafanikio makubwa aliyo ipatia
Arsenal lakini ''CV'' yake inashuka kwa kasi sana na kama atacheza
kama ambavyo tumeishuhudia Arsenal ikicheza mpira mwingi
pasipo kujilinda katika Uefa basi itakuwa dhahma kwa upande wake
mbele ya Mashetani wekundu.
Mpira sio historia kwa maana ya kuipa Manchester United ushindi
lakini Arsenal  matokeo yaweje kama watacheza kwa
wimbi la Manchester hatuwawezagi basi itakula kwao mazima.
Ni hayo tu ngoja tusubiri.

Richard Chardboy: 

Mashabiki wa Arsenal wanakwenda uwanjani wakiwa wamekwishafungwa na mchezo huu. Hawana imani kabisa na timu yao.
Na mashabiki wa Man UTD wanakwenda uwanjani wakiwa wamekwishashinda, hawaoni jinsi gani watafungwa na Arsenal.

Lakini hali ipoje kiuhalisia?
Naamini hali ni tofauti kabisa na fikra za mashabiki kwamba mchezo huu unaweza kua rahisi kwa Man UTD.

Arsenal hawapo hovyo kama wengi wanavyowatazama kwa sababu ya kushika mkia katika kundi lao kwenye UCL.

Narejea kiwango bora walichoonesha dhidi ya Leicester. Leicester ambao walikua hawajapoteza mchezo hata mmoja.

Ni kweli, tishio kubwa kwa Arsenal leo ni kuimarika kwa sehemu ya kiungo ya Manchester UTD chini ya Bastian Schwensteiger ambayo mara nyingi ndiyo ambayo Arsenal hujivunia kuitawala mara nyingi wakikutana na Man UTD (japo huwa wanafungwa).
Lakini siamini kama Sehemu ya kiungo ya Arsenal ikiongozwa na Francis Coquelien itakua dhaifu kiasi cha kuwafanya mashabiki wa Man UTD waamini wamekwishashinda mchezo huu.

Binafsi naamini mechi hii itaamuliwa zaidi na timu itakayokua na nidhamu nzuri ya mchezo, mwanzo mpaka mwisho.

Presha ya kucheza nyumbani ni kubwa kwa Arsenal, japo wana kikosi bora kabisa cha kuweza kupambana na kushinda mechi yoyote duniani, lakini si wazuri sana katika kuhimili presha. Wanaweza kuadhibiwa kwa hili.

Man UTD wanapaswa kucheza zaidi kama timu. wamekua na tatizo la kushindwa kutengeneza nafasi kwa kua kila mmoja anataka kufunga.
Hii inatokana na watu kama Memphis, Martial na Rooney kucheza wakiwa na mzigo mzito wa matarajio ya mashabiki.
Hili linaweza kuwahukumu pamoja na kwamba wapo kwenye kipindi chao cha ubora kwa sasa.

Utabiri wangu...
Arsenal 1-2 Man UTD

No comments

Powered by Blogger.