ISSA HAYATOU AWA RAIS WA FIFA

Kiongozi wa shirikisho la soka barani Afrika Issa Hayatou kutoka Cameroon amepewa jukumu la kuongoza shirikisho la soka duniani Fifa kwa muda.
Hayatou amechukua nafasi ya Sepp Blatter ambaye amesimamishwa kwa siku 90.

Kamati ya Maadili ya shirikisho hilo, shirikisho hilo linalosimamia soka duniani limesema kupitia taarifa. hayatou atachukua usukani kwa mujibu wa sheria za Fifa, akiwa ndiye makamu wa rais katika kamati tendaji ya Fifa aliyehudumu muda mrefu zaidi.

No comments

Powered by Blogger.