STARS YAIPIGISHA KWATA NIGERIA, YAAMBULIA SARE TAIFA

Mbwana Samata na Ali Mustafa wakipiga selfie na Wapenda Soka baada ya mchezo huo
Ikicheza kwa kujiamini na umakini mkubwa Taifa Stars mpya chini ya kocha Mzawa Charles Boniface imeipigisha kwata Nigeria na kutoka suluhu ya bila kufungana katika pambano la kwanza la kundi G baina ya timu hizo katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam.


Mchezo huo ni wa pili kwa Stars katika kutafuta nafasi ya kucheza katika kombe la mataifa ya Afrika maaka 2017 ulishuhudia Stars kupitia kwa washambuliaji wake Mbwana Samata, Tomas Ulimwengu na Mrisho Ngassa wakiisumbua vilivyo ngome ya Nigeria ambayo inanolewa na mchezaji wa zamani wa klabu hiyo Sunday Oliseh.

Kama sio juhudi binafsi za kipa Ikeme Onora kupangua michomo ya washambuliaji wa Stars basi kulikua na kila dalili Stars walikua wanaibuka na ushindi katika pambano hilo.

Kwa matokeo hayo Stars imejikusanyia pointi 1 baada ya kucheza michezo miwili ikishika nafasi ya 3 katika kundi G linaloongozwa na Nigeria wenye pointi 4 wakifatiwa na Misri wenye pointi 3 huku Chard ikikamata nafasi ya mwisho ikiwa haina pointi yoyote.


No comments

Powered by Blogger.