FARU JEURI BINGWA SPORTS EXTRA NDONDO CUP 2015


Mashindano yaliyojizolea umaarufu mkubwa jijini Dar Es Salaam SPORTS EXTRA NDONDO CUP 2015 yamemalizika jioni hii kwa timu ya Faru Jeuri ya Vingunguti kuibuka na ushindi katika mchezo wa fainali dhidi ya Kauzu FC ya Tandika.



Faru Jeuri FC wameibuka na ushindi wa penati 4-3  katika mchezo huo uliopigwa katika dimba la Bandari Tandika jijini Dar es Salaam.

Mchezo huo wa fainali ilibidi uamriwe na matuta baada ya dakika 90 kumalizika kwa sare ya bila kufungana.

Katika mikaaju ya penati Kauzu FC walikosa penati mbili moja ikidakwa na kipa wa Faru FC huku nyingine ikigonga mwamba wakati Faru FC ambao ndiyo mabingwa wao walikosa penati moja ambayo ilidakwa na kipa wa Kauzu FC.






Kifaa kinachotumiwa na Azam Tv kurusha matangazo toka masafa ya juu ambacho leo kilitumika uwanjani hapo

No comments

Powered by Blogger.