TIMU YA VIJANA YAINGIA KAMBINI
Kikosi cha timu ya Taifa cha vijana wenye umri chini ya miaka 15
(U-15) kimeingia kambini katika hosteli za TFF zilizopo Karume kujiandaa na
mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya kombaini ya Morogoro (U-15) mwishoni mwa
wiki hii.
U15 inayonolewa na kocha wake Bakari Shime, ianatarajiwa kucheza
michezo miwili na timu ya kombaoni ya Morogoro (U15) siku ya jumamosi na
jumapili mjini Morogoro, ambapo kocha huyo amekua akitumia nafasi hiyo kupima
uwezo wa vijana wake na kuboresha kikosi kwa kuongeza vijana wengine anaowaona
wanafaa katika timu hiyo.
TFF imekua na program ya timu ya Taifa ya vijana wenye umri
chini ya miaka 15 kukutana kila mwisho wa mwezi kwa kambi, kabla ya kusafiri
mikoani kucheza michezo ya kirafiki. Mpaka sasa timu hiyo imeshacheza na timuza
kombaini za mikoa ya Mbeya na Zanzibar.
Timu hiyo ya vijana wenye umri chini ya miaka 15, inajandaa na kuwania
kufuzu kwa fainali za Mataifa Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17
nchini Madagascar mwaka 2017.
No comments