MASHABIKI WA MANCHESTER UNITED TANZANIA NI ZAIDI YA SOKA WATOA MISAADA HOSPITALI YA MUHIMBILI
Wanaunganishwa na soka huku wakiishabikia klabu ya Manchester United ya England wanajulikana kama Manchester United Supporters in Tanzania Foundation moja ya makundi yanayokuja kwa kasi nchini Tanzania walitumia Jumapili ya jana kutoa misaada kwa wahitaji katika kwa watoto wenye kansa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar Es Salaam.
Akiongea na WAPENDA SOKA blog kiongozi mkuu wa kundi hilo Shaaban Said alisema moyo wa kujitolea walionao wanachama wa kundi hilo ndiyo uliopelekea kufanikisha upatikanaji wa mahitaji hayo na kusisitiza kuwa hawataishia hapo tu lengo ni kusaidia jamii kadri itakavyowezekana na mpango ulio mbele yao ni kuchangia damu siku chache zijazo.
Picha za matukio ya Jana Muhimbili
![]() |
Viongozi wa M.U.S.T Shaban Said kushoto na Mohammed Isimbula wakikabidhi vitu hospitalini hapo |
![]() |
Daktari akitoa maelezo kuhusu historia ya kitengo cha kansa kwa watoto na kujibu maswali toka kwa wanachama |
![]() |
Chicharito akiwa na baadhi ya watoto hospitalini hapo |
No comments