MAN UNITED HAINA JIPYA KWA SWANSEA, YAKUBALI KICHAPO CHA TATU MFULULIZO
Katika hali isiyotegemewa na wengi Swansea City imeendeleza vichapo kwa mabingwa wa kihistoria wa ligi kuu nchini England Manchester United.
Katika mchezo uliopigwa jana jioni katika dimba la Liberty United walikubali kichapo cha bao 2-1 katika mchezo wa raundi ya nne ya ligi kuu nchini England.
Juan Mata alitangulia kufungabao kwa upande wa United kabla ya Andre Ayew hajaisawazishia Swansea na kisha kutoa pasi ya goli la pili lililofungwa na Bafetimbi Gomis na kuzima matumaini ya United kuondoa uteja dhidi ya Swansea ambayo iliifunga mechi zote mbili za msimu uliopita.
UNACHOPASWA KUKIFAHAMU BAADA YA KICHAPO HICHO
- Swansea imeshinda mara 4 kati ya mara 5 zilizopita dhidi ya United katika mashindano yote magoli yote yakiwa ni 2-1
- Mechi mbili za ligi ambazo Manchester United wamepoteza katika ligi wakiwa wametangulia kufunga ni dhidi ya Swansea.
- Ni mechi ya pili Andre Ayew anacheza katika uwanja wa Liberty tangu asajiliwe na katika mechi zote hizo amefanikiwa kufunga bao moja kila mechi.
- Bafetimbi Gomis amefunga goli 9 katika mechi 10 zilizopita katika ligi akiifungia klabu yake ya Swansea.
- Gomis pia ni mchezaji wa kwanza wa Swansea kufunga katika kila mechi katika mechi nne za mwanzo wa ligi.
- Gylfi Sigurdsson ambaye alitoa pasi ya goli la kwanza kwa Swansea ametoa pasi kama hizo za magoli 14 kwa timu hiyo akiwa ndiyo mchezaji pekee kufanya hivyo kwa Swansea.
- Luke Shaw amefanikiwa kutoa pasi ya kwanza ya goli tangu ajiunge na klabu hiyo akicheza jana mechi yake ya 20 kwa Man United.
- Ni mara ya pili tu a Rooney tangu aanze kucheza soka kufikisha mechi ya 10 katika ligi bila goli lolote baada ya kufanya hivyo kati ya mwezi Agosti na Disemba 2003 akiwa na klabu ya Everton.
No comments