CHELSEA YAIADABISHA BARCELONA

Mabingwa wa England Chelsea FC imeibuka na ushindi wa penati 4-2 dhidi ya Mabingwa wa Ulaya na Spain Barcelona katika mchezo wa kuwania kombe la International Champions nchini Marekani.

Mechi hiyo ilibidi iende mpaka katika matuta baada ya kumalizika dakika 90 matokeo yakiwa ni goli 2-2.

Eden Hazard alitangulia kuipatia Chelsea bao la kwanza baada akiipangua ngome ya Barcelona dakika ya 10 kabla ya kufunga na kuwapa Chelsea uongozi na kufanya mechi hiyo kwenda Mapumziko Chelsea wakiwa mbele kwa bao hilo moja.

Luis Suarez aliisawazishia Barcelona dakika ya 52 kabla ya Chipukizi Sandro hajaifungia Barcelona bao la pili na zikiwa zimebaki dakika nne mchezo kumalizika Beki wa Chelsea Gary Cahill alifunga bao la kusawazisha na kufanya mchezo huo kumalizika kwa bao 2-2.

Katika upigaji wa Penati
Inieasta (Barcelona)- alifunga
Flacao (Chelsea) - alifunga
Halilovic (Barcelona) - Alikosa iligonga mwamba
Moses (Chelsea) - Alifunga
Pique (Barcelona) - alikosa iliokolewa na kipa
Ramires (Chelsea) Alifunga
Sandro (Barcelona) - Alifunga
Remy (Chelsea) - Alifunga

Hii ni mechi ya pili mfululizo katika maandalizi Barcelona wanapoteza dhidi ya timu za England.

No comments

Powered by Blogger.