BABA YAKE DALEY BLIND APEWA TIMU YA TAIFA YA UHOLANZI

Danny Blind kushoto akiwa katika benchi la Uholanzi chini ya Hiddink

Huyu ndiye Baba wa mchezaji wa kimataifa wa Uholanzi anagekipiga katika klabu ya Man United Daley Blind ambaye jana alikabidhiwa mikoba ya kuifundisha  timu ya taifa ya Uholanzi.

Mzee huu mwenye miaka 53 naitwa Danny Blind anachukua nafasi ya Guus Hiddink ambaye kazi ya kuifundisha Uholanzi imemshinda na kuamua kubwaga manyanga ikiwa ni miezi kumi tu tangu alipokabidhiwa timu toka kwa Luis Van Gaal.

Danny Blind alikua msaidizi wa kocha Guus Hidink na Luis Van Gaal aliwahi kuichezea Ajax na Sparta Rotterdam na baadae kuifundisha Ajax.

Uholanzi chini ya Hiddink imepoteza michezo mitano nabkushinda michezo minne katika mechi 10 alizoifundisha Uholanzi huku akiicha timu hiyo katika nafasi ya tatu kuwania kufuzu katika michuano ya Ulaya mwakani.


No comments

Powered by Blogger.